Pata taarifa kuu

Kombe la Dunia: Morocco yaichapa Ubelgiji 2-0

Simba wa Atlas wametinga katika mzunguko wa nane baada ya kuwacharaza Ubelgiji kwa mabao 2-0.

Abdelhamid Sabiri, mchezaji wa Morocco akishangilia bao lake dhidi ya Ubelgiji.
Abdelhamid Sabiri, mchezaji wa Morocco akishangilia bao lake dhidi ya Ubelgiji. REUTERS - MATTHEW CHILDS
Matangazo ya kibiashara

Simba wa Atlas kutoka Morocco Jumapili imekuwa timu ya pili ya Afrika kuandikisha ushindi katika michuano ya Kombe la Dunia inayopigwa nchini Qatar  kwa kuifunga Ubelgiji 2-0.

Kwa ushindi huu, Morocco inaongoza kwa muda katika Kundi F.

Kufikia sasa, kati ya nchi tano za Afrika zinazoshiriki michuano ya Kombe hili la Dunia, ni Senegal pekee iliyoandikisha ushindi kwa kuichapa Qatar mabao 3-1.

Mashetani Wekundu watacheza mechi yao ya kufuzu Alhamisi dhidi ya Croatia.

Morocco, washindi kutokana na mabao ya Sabiri (74) na Haboukhlal (90+2) sasa hatima yao iko mikononi mwao: siku nne kabla ya kuburuzana na Canada, wana jumla ya alama nne na wanaweza kujiunga na 16 bora ya michuano hiyo.

Eden Hazard na wachezaji wenzake, ambao tayari walikuwa wameonyesha msisimko mkubwa siku ya Jumatatu licha ya ushindi wa hali ya juu dhidi ya Canada (1-0), wako hatarini, wakiwa na alama tatu pekee. Mafanikio yanaweza kuwa ya lazima dhidi ya Croatia.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.