Pata taarifa kuu

Kombe la Dunia 2022: Ecuador yaibwagiza Qatar katika mechi ya ufunguzi

Timu ya Qatar, nchi mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia la 2022, imeshindwa kufanya vizuri dhidi ya Enner Valencia wa Ecuador ambao wamepata ushindi mabao 2-0 kwenye mechi ya ufunguzi wa michuano hiyo Mwanzo mzuri kwa Waamerika Kusini, na pigo kubwa kwa Qatar, mwenyeji wa michuano hiyo

Enner Valencia, mchezaji wa Ecuador, aliyefunga mabao mawili katika mechi dhidi ya Qatar.
Enner Valencia, mchezaji wa Ecuador, aliyefunga mabao mawili katika mechi dhidi ya Qatar. REUTERS - KIM HONG-JI
Matangazo ya kibiashara

Qatar imejitayarisha kwa maandalizi y michuano ya Kombe la Dunia kwa kipindi cha miaka kumi na miwili . Lakini licha ya kufanya mazoezi bila mashabiki kwa muda wa miezi sita na "dhabihu" za wachezaji "kulazimishwa kufanya mazoezi mbali na familia zao kwa wiki ndefu", Qatar imeshindwa kufanya vizuri katika mechi ya ufunguzi mbele ya mashabiki wake. Pengo lilikuwa kubwa, shinikizo labda lilikuwa kubwa zaidi, na baada ya kuwasili, matumaini yalizamishwa katika nusu ya muda. Raia wa Qatar walitarajia kuwa timu yao itafanya vizuri katika ufunguzi wa michuano hii, lakini "Al Annabi" wamejikuta wakipoteza mechi yao ya kwanza dhidi ya Ecuador. 

Qatar yapoteza

Katika mchezo huu wa ufunguzi, Ecuador hawamkuruhusu mpinzani wao kupata ushindi. Vijana wa Gustavo Alfaro walijizatiti vilivyo kutoka mwanzo wa mechi hiyo. Na ikiwa bao la Enner Valencia, katika dakika ya 3, lilikataliwa baada ya Var kuingilia kati, Ecuador iliishia kutawala baada ya kupata penalti katika dakika ya 16. 

Mechi ya pili ya kundi hili A itapigwa Jumatatu, Novemba 21 saa kumi jioni (UTC) kati ya Uholanzi naa mabingwa wa Afrika, Simba ya Senegal.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.