Pata taarifa kuu
MICHZO-SOKA

Lionel Messi ashinda kwa mara ya saba Tuzo ya kifahari ya Ballon’Or

Lionel Messi, mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka ya Argentina na Paris Saint-Germain nchini Ufaransa ndio mshindi wa mwaka huu wa tuzo ya Ballon d'Or France Football, inayotolewa nchini Ufaransa.

Lionel Messi, mshindi wa Tuzo ya Ballon d'Or 2021.
Lionel Messi, mshindi wa Tuzo ya Ballon d'Or 2021. AFP - FRANCK FIFE
Matangazo ya kibiashara

Hili ni taji la saba la Messi, knyakua taji hili ambalo pia aliwahi kushinda mwaka 2009, 2010, 2011, 2012 ,2015 na 2019.

Messi aliisaidia nchi yake kushinda taji la Copa America, mwezi Julai, taji lake la kwanza la kimataifa, na amefunga magoli 40 mwaka 2021.

Mabao 28 akiifungia Barcelona, manne akiifungia PSG na manane akiifungia Argentina.

Mshambuliaji wa Bayern Munich na Poland Robert Lewandowski alikuwa wa pili, huku kiungo wa kati wa Chelsea na Italia Jorginho akiwa wa tatu.

Raia wa Ufaransa na mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema aliibuka katika nafasi ya nne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.