Pata taarifa kuu
SOKA-PSG

Soka: Lionel Messi awasili Paris kusaini mkataba na PSG

Ndege iliyombeba Lionel Messi, ambayo ilitarajiwa katika mji mkuu wa Ufaransa, Paris, tangu Jumapili, hatimaye imewasili Jumanne hii, Agosti 10 alasiri.

Lionel Messi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Bourget, katika mjini Paris, Jumanne hii, Agosti 10, 2021.
Lionel Messi alipowasili katika uwanja wa ndege wa Bourget, katika mjini Paris, Jumanne hii, Agosti 10, 2021. © REUTERS - YVES HERMAN
Matangazo ya kibiashara

Nyota huyo wa mpira wa miguu sasa anatarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa kiafya kabla ya kusaini mkataba wake na klabu hiyo ya mji mkuu, amethibitisha baba yake na meneja wake, Jorge Messi.

Mkutano na waandishi wa habari utafanyika Jumatano katika jengo la Parc des Princes. Nyota huyo wa soka kutoka Argentina atajiunga, kati ya wengine, na rafiki yake Angel Di Maria na nyota wa Brazil Neymar, ambao wote pamoja waliichezea klabu Barça.

Wengi wanaona kuwa soka imepiga hatu kubwa nchini Ufaransa, baada ya timu za nchi hiyo kufanyiana mikataba na baadhi ya wachezaji nyota duniani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.