Rekodi ya michuano ya soka barani Ulaya
Italia ndio mabingwa wa soka barani Ulaya, baada ya kuishinda Uingereza mabao 3-2 kupitia mikwaju ya penalti, baada ya sare ya bao 1-1 katika mechi ya fainali iliyokwenda hadi katika muda wa ziada katika uwanja wa Wembley, jijini London.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Uingereza ilikuwa ya kwanza kupata bao katika dakika ya 2 ya mchuano huo kupitia Luke Shaw, huku Leonardo Bonucci akisawazisha katika dakika ya 67.
Wachezaji wa Uingereza waliwaacha mashabiki wa nyumbani wakiwa wenye huzuni, baada ya Jadon Sancho, Bukayo Saka na Marcus Rashford kukosa mikwaju ya penalti.
Mabao ya Italia yalitiwa kimyani na Federico Bernardeschi, Leonardo Bonucci na Domenico Berardi kuhakikisha kuwa kombe hilo linakwenda barani Ulaya.
Hii ni fainali ya kwanza, kufika katika hatua ya penalti tangu 1976 wakati Czechoslovakia ilipoishinda Ujerumani.
Hii ni mara ya pili kwa Italia kunyakua taji hili baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza mwaka 1968.
Mwaka 2000 na 2012 ilifika katika hatua ya fainali na kushindwa.
Orodha ya mabingwa wa zamani:-
Ujerumani-1972,1980, 1996
Uhispania-1964, 2008, 2012
Italia-1968, 2020
Ufaransa-1984, 2000
Jamhuri ya muungano wa Soviet-1960
Jamhuri ya Czech-1976
Ureno-2016
Uholanzi-1988
Denmark-1992
Ugiriki-2004