Pata taarifa kuu
ITALIA-MICHEZO

Euro 2020: Italia yakatisha mbio za Uingereza Wembley

Timu ya taifa ya mchezo wa soka ya Italia, ndio mabingwa wa taji la bara Ulaya, baada ya kuishinda Uingereza mabao 3-2 kupitia mikwaju ya penalti katika fainali iliyochezwa usiku wa Jumapili kuamkia leo Jumatatu jijini London.

Kocha Roberto Mancini na wachezaji wake, mabingwa wa Ulaya wakisheherekea ushindi wao, baada ya kuifunga Uingereza kwa mikwaju ya penati (bao 1-1, 3-2) katika fainali ya Euro 2020, Julai 11, 2021 katika uwanja wa Wembley jijini London.
Kocha Roberto Mancini na wachezaji wake, mabingwa wa Ulaya wakisheherekea ushindi wao, baada ya kuifunga Uingereza kwa mikwaju ya penati (bao 1-1, 3-2) katika fainali ya Euro 2020, Julai 11, 2021 katika uwanja wa Wembley jijini London. Michael Regan POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Wananchi wa Italia wameendelea kusherehekea ushindi wao usiku kucha jijini Rome, baada timu yao inayofahamika kama the  Azzuris kutawazwa mabingwa wa soka barani Ulaya, mashindano makubwa yanayotazamwa duniani.

Hili ni taji la pili la Italia, baada ya kushinda mara ya kwanza mwaka 1968.

Hata hivyo, yamekuwa masikitiko kwa Uingereza ambayo ilikuwa inasaka taji lake la kwanza. Mashabiki wa Uingereza waliamini kuwa kombe hilo lingebaki London.

JInsi mchezoulivyokuwa

Baada ya kipindi kigumu cha muda wa ziada ,mshindi hakupatikana timu hzo zilipotoka sare ya bao moja na ikalazimu mikwaju ya penalti kutumiwa kumpata mshindi.

Miaka 15 baada ya Gianluigi Buffon kuisaidia Italia kushinda Kombe la Dunia katika mikwaju ya penati, Gianluigi Donnarumma, mwenye umri wa miaka 22, alifanya hivyo hivyo dhidi ya Uingereza katika fainali ya Euro. Donnarumma aliokoa penati mbili za Saka na Sancho. 

Donnarumma ambaye anahamia Paris Saint-Germain msimu ujao, ametawazwa mchezaji bora wa Euro 2020, na kuwa kipa wa kwanza katika historia ya mashindano hayo kutunukiwa tuzo hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.