Pata taarifa kuu
MICHUANO YA BARA ULAYA-SOKA

Italia yafuzu fainali ya Euro baada ya kuishinda Uhispania

Italia imeifunga Uhispania mabao 4-2 kupitia mikwaju ya penalti baada ya sare ya bao 1-1 katika mchuano wa nusu fainali uliochezwa Jumanne usiku katika uwanja wa Wembley jijini London nchini Uingereza, kutafuta taji la soka barani Ulaya.

Wachezaji wa Italia wakisherehekea ushindi dhidi ya Uhispania katika mechi ya nusu fainali, iliyochezwa Julai 6 2021
Wachezaji wa Italia wakisherehekea ushindi dhidi ya Uhispania katika mechi ya nusu fainali, iliyochezwa Julai 6 2021 Carl Recine POOL/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mechi hiyo ilitawaliwa kwa kisiasi kikubwa na Uhispania hadi katika hatua ya muda wa ziada baada ya mechi hiyo kulazimika kufikia katika kipindi cha mshindi kubainika kwa mikwaju ya penalti.

Italia ndio iliyokuwa ya kwanza kupata bao la ufunguzi kupitia mshambuliaji wake, Federico Chiesa huku Alvaro Morata akiisawazishia Uhispania katika dakika ya 80 ya mchezo huo uliotazamwa na mashabiki karibu 58,000.

Mechi hiyo ilileta kumbukumbu ya nusu fainali ya mwaka 2008 ambayo, Uhispania iliishinda Italia katika kwa mikwaju ya  penalti, lakini mwaka huu ilikuwa mechi ya kulipiza kisasi.

Kufuzu kwa Italia katika hatua ya fainali kumezua shangwe kwa wapenzi wa soka wa wa taifa hilo, na sasa matumaini ni kunyakua taji hilo la bara Ulaya kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1968.

Italia sasa inasubiri mshindi wa nusu fainali ya pili siku ya Jumatano usiku, kati ya Uingereza na Denmark kuelekea fainali ya Jumapili.

Uingereza wakiwa nyumbani, wana matumaini ya kufika katika fainali kubwa ya mchezo wa soka tangu iliponyakua kombe la dunia mwaka 1966.

Mwaka 1996 Uingereza pia ilifika katika hatua hii ya nusu fainali na matokeo mazuri ilipata mwaka 1968 ilipomaliza katika nafasi ya tatu.

Denmark nayo inakwenda katka mechi hii muhimu ikiwa na kumbukumbu ya kushinda taji hili mwaka 1992. Mwaka 1984 wakati michuano hii ilipofanyika nchini Ufaransa, ilifika pia katika hatua ya nusu fainali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.