Pata taarifa kuu
CAF-SOKA

Mechi za robo fainali kuwania taji la vijana wasiozidi miaka 20 kunguruma

Mechi za robo fainali kuwania taji la soka kwa vijana wasiozidi miaka 20 inaanza kuchezwa siku ya Alhamisi nchini Mauritania.

Mechi iliyopita, kati ya Uganda na Mauritania, iliyochezwa tarehe 20 , Februari 2021.
Mechi iliyopita, kati ya Uganda na Mauritania, iliyochezwa tarehe 20 , Februari 2021. © Courtesy of CAF
Matangazo ya kibiashara

Mechi ya kwanza, itakuwa gani ya Cameroon na Ghana, mchuano unaotarajiwa kuwa na ushindani mkali, katika uwanja wa Olympique jijini Nouakchott.

Ghana wanaocheza katika mashindano haya mara ya 12, wanatafuta taji la nne, tangu waliposhinda mara ya mwisho mwaka 2009.

Cameroon, nao wanaoshiriki kwenye michuano ya 10 wanasaka taji lake la pili kwa mara ya kwanza ndani ya miaka 26.

Morocco  nayo itachuana na Tunisia katika mechi nyingine.

Mechi ya robo fainali, Februari 26 2021:-

Burkina Faso vs Uganda

Jamhuri ya Afrika ya Kati vs Gambia

 

Fainali itachezwa tarehe 6  mwezi Machi mwaka 2021.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.