Pata taarifa kuu
CAF-SOKA-TUZO

Mohammed Salah mchezaji bora wa mchezo wa soka barani Afrika

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka ya Misri na klabu ya Liverpool nchini Uingereza, Mohammed Salah, kwa mara ya pili mfululizo amepata tuzo ya mchezo bora barani Afrika.

Mchezaji bora wa soka barani Afrika Mohamed Salah (Katikatie), akiwa na rais wa CAF Ahmad Ahmad (Kushoto)  na Liberia George Weah (Kulia)
Mchezaji bora wa soka barani Afrika Mohamed Salah (Katikatie), akiwa na rais wa CAF Ahmad Ahmad (Kushoto) na Liberia George Weah (Kulia) RFI / Pierre René-Worms
Matangazo ya kibiashara

Salah mwenye umri wa miaka 26, amepata tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika usiku wa kuamkia leo jijini Dakar nchini Senegal na kuwashinda Sadio Mane, anayecheza naye klabu moja lakini pia Pierre-Emerick Aubameyang raia wa Gabon anayecheza soka katika klabu ya Arsenal.

Mshindi huyo amesema, tuzo hiyo inaitoa kwa ajili ya taifa lake la Misri, lakini pia bidii aliyoionesha katika klabu yake na timu yake ya taifa ndio imemsaidia kupata tuzo hiyo.

“Nimekuwa na ndoto ya kushinda taji hili, tangu nilipokuwa mtoto na sasa hivi nimeshinda mara mbili mfululizo, “ amesema Salaha baada ya kupata tuzo hiyo.

“Naishukuru sana familia yangu, wachezaji wenzangu na mashabiki, naitoa tuzo hii kwa nchi yangu ya Misri,” alisema.

Tuzo za mchezaji bira barani Afrika, hutolewa kila mwaka, tangu mara ya kwanza mwaka 1970.

Historia ya wachezaji waliowahi kushinda taji hili ni pamoja na Abedi 'Pele' Ayew (Ghana), Samuel Eto'o (Cameroon, Yaya Toure (Ivory Coast), wote wameshinda mara nne, huku George Weah kutoka Liberia, akisinda mara tatu.

Wachezaji wengine waliowahi kushinda taji hili mara mbili ni pamoja na Roger Milla, Thomas N'Kono (wote kutoka Cameroon ), El Hadji Diouf (Senegal), Didier Drogba (Ivory Coast), Nwankwo Kanu (Nigeria) na sasa Mohamed Salah (Misri).

Orodha kamili:

Mchezaji bora wa mwaka- Mohamed Salah (Misri, Liverpool)

Mchezaji bora kwa upande wa wanawake-Chrestinah Kgatlana (Afrika Kusini)

Mchezaji chipukizi wa mwaka-Achraf Hakimi (Morocco)

Kocha bora wa mwaka- Herve Renard (Morocco)

Kocha bora kwa upande wa wanawake-Desiree Ellis (Afrika Kusini)

Timu bora ya mwaka-Mauritania

Timu bora kwa upande wa wanawake-Nigeria

Bao bora la mwaka-Chrestinah Kgatlana (Afrika Kusini)

Kikosi bora cha soka Afrika-

Denis Onyango (Uganda); Serge Aurier (Ivory Coast), Medhi Benatia (Morocco), Eric Bailly (Ivory Coast), Kalidou Koulibaly (Senegal), Thomas Partey (Ghana), Naby Keita (Guinea), Riyad Mahrez (Algeria); Sadio Mane (Senegal), Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon), Mohmaed Salah (Misri)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.