Pata taarifa kuu
MISRI-CAF-SALAH-SOKA

Mohammed Salah atunukiwa tuzo ya mchezaji bora wa Mwaka

Mshambuliaji wa timu ya taifa ya soka ya Misri na klabu ya Liverpool nchini Uingereza, Mohammed Salah kwa mara ya pili mfululizo amepata tuzo ya mchezo bora barani Afrika.

Mohammed Salah, mchezaji bora barani Afrika
Mohammed Salah, mchezaji bora barani Afrika www.cafonline.com
Matangazo ya kibiashara

Salah mwenye umri wa miaka 26, amepata tuzo hiyo katika hafla iliyofanyika usiku wa kuamkia leo jijini Dakar nchini Senegal na kuwashinda Sadio Mane, anayecheza naye klabu moja lakini pia Pierre-Emerick Aubameyang raia wa Gabon anayecheza soka katika klabu ya Arsenal.

Salah aliwafungia Liverpool mabao 44 msimu wa 2017-18 na kuisaidia klabu hiyo kufika fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ingawa walishindwa na Real Madrid.

Amefunga mabao 16 katika mechi 29 alizoichezea Liverpool mashindano yote msimu huu.

Salah, Mane na Aubameyang wamo kwenye kikosi bora cha Mwaka Afrika pamoja na beki wa Manchester United Eric Bailly, kiungo wa kati wa Manchester City Riyad Mahrez, kiungo wa kati wa Liverpool Naby Keita na beki wa kushoto wa Tottenham Serge Aurier.

Kwa upande wa wanawake, mshambuliaji wa Houston Dash kutoka Afrika Kusini Thembi Kgatlana alitawazwa mchezaji Bora wa Mwaka wa kike.

Tuzo za mchezaji barani Afrika, hutolewa kila mwaka.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.