Pata taarifa kuu
KOREA KUSINI-KOREA KASKAZINI-USHIRIKIANO

Maafisa wa Korea Kusini ziarani Korea Kaskazini

Ujumbe wa Korea Kusini umekwenda Korea Kaskazini kuthathmini viwanja vitakavyotumiwa kufanya maandalizi ya kushiriki katika michezo ya Olimpiki msimu wa baridi mwezi ujao.

Wachezaji maarufu wa mchezo wa magongo kutoka Korea Kaskazini  (hapa ilikua mwaka 2003).
Wachezaji maarufu wa mchezo wa magongo kutoka Korea Kaskazini (hapa ilikua mwaka 2003). KIM JAE-HWAN/AFP
Matangazo ya kibiashara

Mataifa hayo mawili, mapema mwezi huu yalikubaliana kuunda timu moja ya mchezo wa magongo lakini pia kuandamana pamoja wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo nchini korea Kusini.

Hata hivyo, makubaliano haya, yamewakera baadhi ya raia wa Korea Kaskazini ambao wameandamana na kuchoma picha za kiongozi wao Kim Jong un na kumwita, msaliti.

Mashindano hayo yatazinduliwa Februari 9.

Seoul ilitafuta kwa muda mrefu kuonesha tukio hili kama "Michezo ya Amani" katika mazingira ya uhasama kuhusu mpango wa nyuklia wa Korea Kaskazini na majaribio ya kombora ya masafa marefu.

"Uhusiano kati ya Korea mbili ulikua si mzuri kwa karibu miaka 10," alisema kiongozi wa ujumbe wa Korea Kaskazini katika mazungumzo hayo, Jon Jong-Su. Mazungumzo kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini yalifanyika katika mji wa Panmunjom, ulio kwenye mpaka kati ya Korea mbili.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.