Pata taarifa kuu
BARCELONA-SOKA-MICHEZO

Barcelona yamteua Ernesto Valverde kuwa meneja mpya

Klabu ya Barcelona imemteua Ernesto Valverde kuwa meneja mpya wa wachezaji wa klabu hii kwa mkataba wa miaka miwili. Bw valverde anaweza akaongezewa mwaka mwingine wa tatu, imse a taarifa kutoka klabu ya Barcelona.

Wachezaji wa FC Barcelona wakishangilia baada ya mchezo wao na PSG ambapo wameweka historia kwenye michuano hiyo. Machi 8, 2017.
Wachezaji wa FC Barcelona wakishangilia baada ya mchezo wao na PSG ambapo wameweka historia kwenye michuano hiyo. Machi 8, 2017. Reuters / Albert Gea Livepic
Matangazo ya kibiashara

Rais wa Barca Josep Maria Bartomeu alimsifu Valverde, 53, kwa uwezo wake, ufahamu, ujuzi na busara na kusema anaendeleza wachezaji chipukizi na hucheza mtindo wa Barca.

Valverde atazinduliwa rasmi kama meneja wa Barca siku ya Alhamisi wiki hii.

Ernesto Valverde anachukua nafasi ya Luis Enrique aliyetangaza mnamo mwezi Machi kwamba angeihama klabu hiyo iliyomaliza nafasi ya pili La Liga msimu huu.

Enrique aliongoza Barcelona kushinda mataji matatu makuu msimu wake wa kwanza, mataji mawili makuu ya nyumbani mwaka 2016 na Kombe la Mfalme (Copa del Rey) mwaka huu.
Bw Enrique anaondoka baada ya kumaliza mkataba wake wa miaka mitatu.

Valverde ni mshambuliaji wa zamani wa Barca na alitangaza wiki iliyopita kwamba angeacha kazi Athletic Bilbao baada ya kuwaongoza kwa miaka minne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.