Pata taarifa kuu
UHISPANIA-REAL MADRID-BARCA

Real Madrid yanyakua ubingwa wa la Liga mbele ya Barca

Jumapili Mei 21 Real Madrid imetwaa taji la 33 la mabingwa wa soka la Uhispania katika historia yake. Real Madrid ilipata ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Malaga wakati wa mchezo wa mwisho wa michuano ya ligi kuu ya Uhispania (La Liga), ikiongozi dhidi ya Barcelona, ambao walishinda Eibar kwa mabao 4 -2.

Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo.
Mshambuliaji wa Real Madrid Cristiano Ronaldo. Reuters / Jon Nazca
Matangazo ya kibiashara

Real Madrid ilipata taji lake la taifa baada ya miaka mitano ya kusubiri. Klabu hii ilijiongeza taji la 33 mabingwa wa soka nchini Uhispania (rekodi mpya) kwa orodha yao kubwa baada kupata tuzo la 32 mwaka 2011 -2012.

Madrid ilikua ikihitaji alama moja kabla ya mchezo huo walianza kupata bao la kuongoza katika dakika ya pili ya mchezo kupitia kwa Cristiano Ronaldo, kisha Karim Benzema akifunga bao la pili katika dakika ya 55.

Mshambuliaji wa Barcelona Lionel Messi amekuwa mfungaji bora wa ligi hiyo akimaliza na mabao 37, akifuatiwa na Luis Suarez, mwenye mabao 29, Cristiano Ronaldo akiwa katika nafasi ya tatu kwa magoli 25.

Madrid imemaliza msimu ikiwa na alama 93 kwa michezo 38 ikifuatiwa na hasimu wake Barcelona iliomaliza na alama 90 baada ya ushindi wa mabao 4-2 dhidi ya Eibar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.