Pata taarifa kuu
SOKA-FIFA

Brazil yarejea katika uongozi wa soka baada ya miaka 7

Brazil imerejea kileleni kama  taifa bora katika mchezo wa soka dunia, kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010.

Wachezaji wa Brazil wakisherehekea ushindi baada ya kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2018
Wachezaji wa Brazil wakisherehekea ushindi baada ya kufuzu kucheza kombe la dunia mwaka 2018 REUTERS/Nacho Doce
Matangazo ya kibiashara

Hiii imebainika baada ya Shirikisho la soka duniani FIFA kutoa orodha ya mataifa bora katika mchezo wa soka kwa mwezi wa Machi.

Hatua hii imekuja baada ya Brazil kuwa nchi ya kwanza, kufuzu katika fainali ya kombe la dunia mwaka 2018 wiki iliyopita.

Tangu mwaka 2010 baada ya kombe la dunia nchini Afrika Kusini na kuondolewa mapema, katika michuano hiyo.

Nafasi ya pili imekwenda kwa Argetina.

Mabingwa wa dunia ni Ujerumani katika nafasi ya tatu, huku Chile ikiwa ya nne na Colombia kufunga tano bora.

Uhispania iliyokuwa wakati mmoja nambari sasa ni ya 10.

Barani Afrika, Misri ni ya kwanza lakini ni ya 19 duniani ikifuatwa na Senegal ambayo ni ya 30 duniani.

Burkina Faso ni ya tatu na ya 35 duniani huku Nigeria ikifunga nne bora na ya 40 duniani.

Katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati, Uganda inaendelea kuongoza baada ya kupanda nafasi mbili na sasa ni ya 72 duniani.

Inafuatwa na Kenya ambayo imepanda nafasi 10 na sasa ni ya 78 duniani.

Tanzania imepanda nafasi 22, na sasa ni ya 135 duniani, huku Rwanda ikishuka nafasi hadi katika nafasi ya 117 duniani na baada ya kushuka nafasi 24.

Ethiopia ambayo imeshuka nafasi 20, ni ya 124 huku Burundi ikiwa ya 141 baada ya kushuka nafasi mbili.

Mabadiliko haya yamekuja baada ya michuano kadhaa ya kirafiki mwishoni mwa mwezi Machi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.