Pata taarifa kuu
MICHUANO YA KOMBE LA DUNIA

Brazil yasalimu amri mbele ya Ujerumani

Ni kilio, huzuni kwa wachezaji wa mashabiki wa soka wa Brazil baada ya kufungwa na Ujerumani mabao 7 kwa 1 katika hatua ya nusu fainali ya kombe la dunia.

David Luiz en larmes à l'issue de la lourde défaite du Brésil en demi-finale face à l'Allemagne.
David Luiz en larmes à l'issue de la lourde défaite du Brésil en demi-finale face à l'Allemagne. REUTERS/David Gray
Matangazo ya kibiashara

Wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil, Marcelo na Oscar wakijaribu kumzuia mshambuliaji wa Ujerumani, Müller karibu na lango la Brazil.
Wachezaji wa timu ya taifa ya Brazil, Marcelo na Oscar wakijaribu kumzuia mshambuliaji wa Ujerumani, Müller karibu na lango la Brazil. REUTERS/Kai Pfaffenbach

Mshambuliaji, Thomas Muller ndiye aliyekuwa wa kwanza kuipa timu yake bao katika dakika ya 11 ya mchezo huo, kabla ya Miroslav Klose kufunga bao la pili. Muller amesema hajaamini kwamba Brazil ndio iliyofungwa mabao hayo yote, na kubaini kwamba mchezo ni ule ule kwa timu itakayokutana na Ujerumani katika fainali.

“Siamini macho yangu, kwamba kweli Brazili ndio imefungwa mabao 7-1, amesema Müller, mshambuliaji kiungo wa Brazil, mwenye umri wa miaka 24. Mchezaji huyo amebaini kwamba hawakutaraji kwamba Ujerumani itafunga mabao yote hayo.

“Kuna tofauti kubwa kati ya mchezo huu na ule tuliocheza na Algeria, kwani tumemiliki mpira kwa asilimia kubwa, na kipindi cha kwanza tumetawala mpira. Hii inaonesha kuwa hakuna bingwa wa soka, kila kitu kinawezekana, amesema Thomas Müller.

Ndani ya muda wa sekunde 179, Toni Kross aliifungia timu yake mabao 2 huku Sami Khedira akifunga bao la 5 kufikia mwisho wa kipindi cha kwanza.

Sami Khedira akikabiliana na wachezaji wa Brazil, Dante na David Luiz.
Sami Khedira akikabiliana na wachezaji wa Brazil, Dante na David Luiz. REUTERS/Eddie Keogh

Mshambuliaji wa Chelsea Andre Schurrle, aliyeingia katika kipindi cha pili aliifungia Ujerumani mabao mawili na kufikisha idadi ya mabao kuwa 7.

Mashabiki wa Brazil hawakuamini macho yao, ilikuwa ni machozi na huzuni huku wakiondoka uwanjani kwa masikitiko makubwa huku wengine wakisema kukosekana kwa Neyma na nohodha Silva Thiago kulichangia matokeo kuwa mabaya.

Bao la dakika ya 90 la Oscar, angalau liliwafuta machozi wachezaji wa kocha Luiz Felipe Scholari ambaye amesema siku ya Jumanne ilikuwa siku ngumu sana katika maisha yake, na ameomba msahama mashabiki wa nchi hiyo.

Golikipa wa Brazil,  Julio Cesar akikataa tamaa baada ya bao la Miroslav Klose.
Golikipa wa Brazil, Julio Cesar akikataa tamaa baada ya bao la Miroslav Klose. REUTERS/Marcos Brindicci

Mara ya mwisho Brazil kufungwa mabao mengi kama haya ilikuwa mwaka 1920 wakati wa michuano ya Copa America ambapo walifungwa mabao 6 kwa 0 dhidi ya Uruguay.

Hii ndio mara ya kwanza kwa timu kufungwa au kufunga mabao 7 katika michuano ya kombe la dunia tangu mwaka 1954 ambapo Ujerumani walipowashinda Austria mabao 6 kwa 1 katika michuano hii.

Ujerumani imekuwa timu ya kwanza kufunga mabao 5 kwa muda wa dakika 29 katika historia ya michuano hii lakini pia imevunjika rekodi ya Brazil kwa kuwa na mabao mengi katika historia ya michuano hii.Hadi sasa ina mabao 223.

Miroslav Klose akivunja rekodi wa kufunga mabao.
Miroslav Klose akivunja rekodi wa kufunga mabao. REUTERS/Marcos Brindicci

Mshambuliaji wa Ujerumani Miroslav Klose ameweka hitoria kwa kuwa mchezaji ambaye amefunga mabao mengi katika kombe la dunia hadi sasa akiwa na mabao 16 katika michuano 23 na kumpita Ronaldo aliyekuwa anashikilia rekodi hiyo na mabao 15.
Brazil sasa itamenyana na Argentina au Uholanzi kumtafuta mshindi wa tatu siku ya Jumamosi.

Ushindi huu wa Ujerumani dhidi ya Brazil umepelekea watu milioni 35.6 kutembelea mtandao wa kijamii wa Twitter na kutoa maoni yao. Hali hii inaonesha ni kiasi gani watu wamekua wakifuatilia michuano ya kombe la dunia.

Kwa mara ya kwanza idadi kubwa ya watu waliyotembelea mtandao wa kijamii wa Twitter na kutoa maoni yao, ni katika michuano ya kombe la 48 nchini Marekani (Super Bowl) iliyochezwa mwezi februari mwaka huu, ambapo watu milioni 25 kutoa maoni yao kuhusu michuano hiyo.

Bao la tano liliyofungwa na mchezaji, Sami Khedira, baada ya dakika sita kuwekwa wavuni bao la nne, liliyofungwa na Mannschaft, lilipelekea watu 580.166 kutoa maoni yao kwa muda wa dakika moja.

 

Uwanja wa Mineirao katika mji wa  Belo Horizonte kabla ya mchuano kati ya Brazil na Ujerumani, Julai 8 mwaka 2014.
Uwanja wa Mineirao katika mji wa Belo Horizonte kabla ya mchuano kati ya Brazil na Ujerumani, Julai 8 mwaka 2014. REUTERS/Leonhard Foeger

Mchuano mwingine wa nusu fainali Jumatano usiku, Argentina inachuana na Uholanzi.

Huenda mshambulizi wa Uholanzi Robin van Persie asicheze mechi ya leo kwa kusumbuliwa na tumbo, hata hivyo kiungo wa kati Nigel de Jong baada ya kupona jeraha.

Argentina itamkosa kiungo wake wa kati Angel Di Maria ambaye anasumbuliwa na jeraha la paja lakini huenda akaanza mchuano wa leo.

Kocha wa Uholanzi Loius Vaan Gaal anawategemea wachezaji kama Arjen Robben, Wesley Sneijder, Nigel del Jong ambao ni viungo wakabaji kukaba na kutafuta mabao.

Mchezaji mwengine pia wakutegemewa katika mchuano huu ni Dirk Kuyt.

Dirk Kuyt jubile, mchezaji wa Uholanzi.
Dirk Kuyt jubile, mchezaji wa Uholanzi. Reuters

Kwa upande wa Argentina kocha Alejadro Sabella amekuwa anamtegemea mshmabuliaji na nahodha Lionel Messi kuongoza mashambulizi kwenda ngome ya Uholanzi wachezaji wengine wa kuangalia ni pamoja na Sergio Aguero na Gonzalo Huguan.

Licha ya kutokuwepo kwa Angel di Maria, watakuwa wanawategemea wachezaji kama Fenando Gago , Pablo Zabaleta amabye ni beki pamoja na Marcos Rojo.

Mara ya mwisho timu hizi kukutana ilikuwa ni mwaka 2006 katika michuano ya kombe la dunia ambapo walitoka sare ya kutofungana.

Hii ni nusu fainali ya kwanza ya Argentina tangu mwaka 1990.

Historia inaonesha kuwa hawajawahi kushgindwa katika mchuano wowote wa nusu fainaki katika michuano ya kombe la dunia.

Kwa upande wa Uholanzi hii ni nusu fainali yake ya tatu katika michuano minne ya kombe la dunia zilizopita.
Mwaka 2010 walifika katua hatu ya fainali nchini Afrika Kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.