Pata taarifa kuu
AFCON 2019

Mechi za soka kufuzu fainali ya AFCON 2019 zaanza kutifua vumbi

Mataifa manne yanashuka dimbani siku ya Jumatano, kumenyana katika mchuano muhimu wa soka hatua ya awali, kutafuta nafasi ya kufuzu hatua ya makundi kuwania ubingwa wa bara Afrika mwaka 2019 nchini Cameroon.

Mabingwa taji la AFCON mwaka 2017.
Mabingwa taji la AFCON mwaka 2017. GABRIEL BOUYS / AFP
Matangazo ya kibiashara

Sao Tome and Principe ipo nyumbani kumenyana na Madagascar, huku Djibouti ikipambana na Sudan Kusini.

Sudan Kusini inashiriki katika michuano ya kufuzu kucheza fainali za Afrika kwa mara ya tatu tangu nchi hiyo ilipopata uhuru wake mwaka 2011.

Mechi za marudiano ni siku ya Jumapili wiki hii.

Mshindi baada ya mechi zote mbili atafuzu katika hatua ya makundi.

Siku ya Ijumaa, Comoros nao watakuwa nyumbani mjini Moroni kumenyana na Mauritius, huku mchuano wa marudiano ukipangwa kufanyika mapema wiki ijayo.

Mshindi kati ya Sao Tome and Principe na Madagascar, atafuzu katika kundi la A ambalo lina Senegal, Equatorial Guinea na Sudan.

Naye mshindi kati ya Sudan Kusini na Madgascar atafuzu kucheza katika kundi la B, pamoja na Cameroon, Morocco na Malawi.

Nalo kundi la C ambalo tayari lina Mali, Gabon, Burundi na Burundi linamsubiri mshindi kati ya Comoros na Mauritius.

Hata hivyo, katika mechi zote za kufuzu miaka iliyopita, imekuwa ikifanya vibaya na kufungwa mabao 15. Imefanikiwa tu kufunga bao 1.

Mechi za hatua ya makundi zitaanza kutifua vumbi mwezi Juni mwaka huu na kumalizika mwaka 2018 mwezi Novemba.

Mshindi wa kwanza atafuzu katika fainali hizo pamoja na timu zingine tatu zitakazokuwa zimemaliza katika nafasi ya pili lakini kwa alama nzuri.

Kuna makundi 12, na kila kundi lina timu nne.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.