Pata taarifa kuu
ROONEY

Wachezaji wa timu ya taifa ya Uingereza wamtetea Rooney baada ya kuzomewa na mashabiki

Wachezaji wa Uingereza bado wana mshangao mkubwa baada ya sehemu ya mashabiki wa timu ya taifa ya Uingereza waliokuwa wakishuhudia timu yake ikicheza mchezo wa kufuzu kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi, kumzomea nahodha wa timu hiyo, Wayne Rooney.

Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Wayne Rooney akiwapa ishara ya dole mashabiki wa timu yake ya taifa wakati wa mchezo dhidi ya Malta ambapo aliiongoza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, 8 October 2016.
Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Wayne Rooney akiwapa ishara ya dole mashabiki wa timu yake ya taifa wakati wa mchezo dhidi ya Malta ambapo aliiongoza kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, 8 October 2016. Reuters / Stefan Wermuth Livepic
Matangazo ya kibiashara

Mwishoni mwa juma Uingereza ilikuwa ikicheza na Malta kwenye dimba la Wimbley na kuibuka na ushindi wa mabo 2-0, lakini mara baada ya mchezo huo mashabiki wa Uingereza walianza kumzomea Rooney.

Rooney ambaye amefunga goli moja tu katika michezo 12 ya klabu yake ya Manchester United na timu yake ya taifa ya Uingereza msimu huu, alijikuta akizomewa na kikundi cha mashabiki waliokuwa Wimbley wakati akicheza kwenye sehemu ya kiungo.

Hata hivyo wachezaji wenzake wameeleza kushtushwa na kitendo kilichooneshwa na mashabiki hao, ambapo beki wa kati ya Uingereza na klabu ya Manchester City, John Stone, amesema Rooney alicheza vizuri na anashangaa kuona mashabiki waliamua kumzomea.

Kiungo Jordan Henderson amesema kuwa nahodha wao alionesha kiwango kikubwa kwenye safu ya kiungo ya timu hiyo, na hakustahili kufanyiwa alichofanayiwa na mashabiki.

Nafasi anayocheza Wayne Rooney kwenye timu yake ya taifa imezua maswali mengi hivi karibuni, ambapo sasa huchezeshwa zaidi sehemu ya kiungo kutokana na nafasi yake ya kawaida ya ushambuliaji kuwa na wachezaji mahiri kama Harry Kane, Daniel Sturridge na dele Alli.

Rooney pia amejikuta akianzia benchi kwenye klabuj yake katika michezo mitatu mfululizo ya ligi kuu ya Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.