Pata taarifa kuu
EURO 2016

Tulieni tutaondolewa mashindanoni, Rooney awaambia mashabiki

Nahodha wa timu ya taifa ya Uingereza, Wayne Rooney na kocha mkuu wa timu hiyo, Roy Hodgson, wametoa wito kwa mashabiki wa timu hiyo kuwa watulivu na kujiepusha na vitendo vya vurugu ili kuepuka kuchukuliwa hatua na kuondoshwa kwenye michuano ya mwaka huu nchini Ufaransa. 

Nahodha wa Uingereza, Wayne Rooney akiwa na kocha wake Roy Hodgson, ambapo wametoa wito kwa mashabiki kuwa watulivu
Nahodha wa Uingereza, Wayne Rooney akiwa na kocha wake Roy Hodgson, ambapo wametoa wito kwa mashabiki kuwa watulivu Reuters / Pool Pic / UEFA Livepic
Matangazo ya kibiashara

"Ninawaomba mjiepushe na vurugu," amesema Hodgson kwenye mkanda wa video uliotolewa na chama cha soka Uingereza, kocha huyo amesema kuwa "Sote tunahitaji sana kubakia kwenye michuano hii."

Kwa upande wake nahodha wa timu hiyo, Wayne Rooney amewaambia mashabiki kuwa "Kuweni makini, salama na muendelee kutuunga mkono kwa nguvu kubwa zaidi kama mlivyoonesha kwenye mechi yetu ya ufunguzi."

Baada ya vurugu zilizojitokeza mjini Marseille mwishoni mwa juma na kuharibu raha iliyoshuhudiwa wakati wa mchezo kati ya Uingereza na Urusi ambazo zilitoka sare ya bao 1-1, shirikisho la mpira Ulaya, UEFA limetishia kuzitupa nje ya mashindano timu hizi ikiwa hali iliyoshuhudiwa mwishoni mwa juma itaendelea.

Shirikisho la Ulaya pia lilizitaka nchi zote mbili kutoa wito kwa mashabiki wao kujiepusha na vurugu.

Uingereza inatarajiwa kushuka dimbani siku ya Alhamisi kuwakabili mahasimu wao timu ya taifa ya Wales mjini Lens, ambapo Urusi nao watakuwa uwanjani kucheza na Slovaki kwenye mji wa Lille siku moja kabla.

Katika hatua nyingine mashabiki zaidi ya 10 wamefunguliwa mashtaka nchini Ufaransa kutokana na vurugu zilizojitokeza mwishoni mwa juma lililopita kwenye mechi kati ya Urusi na Uingereza, huku mwendesha mashtaka akisema kuwa zaidi ya mashabiki 150 wa Urusi hawajakamatwa.

Shabiki mmoja pia wa Ireland ya Kaskazini mara baada ya mchezo wao dhidi ya Polans hapo jana, alifariki dunia baada ya kuangukia mtoni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.