Pata taarifa kuu
OLIMPIKI-BRAZIL 2016-RIADHA

Faith Kipyegon aishindia Kenya medali ya dhahabu katika mbio za Mita 1500

Mkenya Faith Kipyegon ameishindia nchi yake medali ya dhahabu katika mbio za Mita 1500 kwa upande wa wanawake katika Michezo inayoendelea ya Olimpiki nchini Brazil.

Mkenya Faith Kipyegon alivyoshinda mbio za Mita 1500
Mkenya Faith Kipyegon alivyoshinda mbio za Mita 1500 athleticsweekly.com
Matangazo ya kibiashara

Kipyegon mwenye umri wa miaka 22, alishinda mbio hizo kwa muda wa dakika 4, sekunde 08 nukta 92 na kumshinda Genzebe Dibaba kutoka Ethiopia anayeshikilia rekodi ya dunia.

Faith Kipyego baada ya kushinda medali ya dhahabu Mita 1500 katika Michezo ya Olimpiki nchini Brazil Agosti 17 2016
Faith Kipyego baada ya kushinda medali ya dhahabu Mita 1500 katika Michezo ya Olimpiki nchini Brazil Agosti 17 2016 Daily Nation

Mwanariadha huyo anasema alifahamu kuwa alikuwa na ushindani mkali sana na alilazimika kutumia nguvu na maarifa katika mita za mwisho 250 na kumshinda Dibaba aliyemaliza wa pili kwa muda wa dakika 4 sekunde 10 nukta 27.

Aidha, Kipyegon ambaye ameshiriki katika michezo ya Olimpiki kwa mara ya kwanza, ameongeza kuwa kuelekea kwenye mashindano haya alijiandaa vema sana na anajivunia kuishinda nchi yake medali ya dhahabu.

Faith Kipyego akisherehekea baada ya kushinda medali ya dhahabu Mita 1500 katika Michezo ya Olimpiki nchini Brazil Agosti 17 2016
Faith Kipyego akisherehekea baada ya kushinda medali ya dhahabu Mita 1500 katika Michezo ya Olimpiki nchini Brazil Agosti 17 2016 Daily Nation

Nafasi ta tatu ilimwendea Mmarekani Jennifer Simpson aliyemaliza kwa muda wa dakika 4, sekunde 10 nukta 53.

Kenya sasa inashikilia nafasi ya 16 duniani na ni ya kwanza barani Afrika, baada ya kupata medali 3 za dhahabu, zingine tatu za fedha na jumla kuwa na medali 6.

Marekani inaendelea kuongoza jedwali hilo kwa kuwa na medali 84, 28 zikiwa za dhahabu ikifuatwa na Uingereza ambayo ina medali 50 ikiwa ni pamoja na 19 za dhahabu.

Kenya inatarajiwa kufanya vizuri Alhamisi hii katika mbio zingine za Mita 3000, kuruka viunzi na maji kwa upande wa wanaume, mbio ambazo imekuwa ikitawala kwa muda mrefu sasa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.