Pata taarifa kuu
RIO OLIMPIKI 2016

Rudisha atetea ubingwa wake, Miller amaliza kishujaa, mchezaji wa Misri afukuzwa

Mwanariadha wa Kenya, David Rudisha, amefanikiwa kutetea ubingwa wake wa mita 800 kwa upande wa wanaume, baada ya kushinda mbio hizo kwenye michezo ya Rio, Brazil, huku katika mbio za mita 400 wanawake, mwanariadha wa Bahamas Shaunae Miller akishinda medali ya dhahabu kwa staili ya aina yake.

Le Kényan David Rudisha.
Le Kényan David Rudisha. REUTERS/Lucy Nicholson
Matangazo ya kibiashara

Rudisha mwenye umri wa miaka 27, alionesha uzoefu wake katika mbo hizo kwa kutoonesha papara dhidi ya Mkenya mwenzake Alfred Kipketer aliyewaacha mwanzo tu wa mbio.

Rudisha aliongeza kasi zikiwa zimesalia mita 300 kumaliza ambapo Kipketer alianza kuishiwa pumzi na kumpa nafasi Rudisha kushinda mbio hizo kwa muda wa dakika moja sekunde 42 nukta 15.

Mkenya, David Rudisha akiwa na Mu Algeria Taoufik Makhloufi na Mmarekani Clayton Murphy, baada ya mbio za mita 800 jijini Rio, Brazil, 15AUG2016
Mkenya, David Rudisha akiwa na Mu Algeria Taoufik Makhloufi na Mmarekani Clayton Murphy, baada ya mbio za mita 800 jijini Rio, Brazil, 15AUG2016 REUTERS/Leonhard Foeger

Mu Algeria Toufik Makhloufi alishinda medali ya fedha huku Mmarekani Clayton Murphy akishinda medali ya shaba.

Mwanariadha wa Kenya, Kipketer alianza mbio hizo kwa kasi ya aina yake katika mita 200 za kwanza akitumia sekunde 23 pekee, mwanariadha huyu mwenye umri wa miaka 19, alimshinda Rudisha wakati wa majaribio ya kufuzu kwenda Rio.

Ushindi wa Rudisha unamfanya kuwa mwanamichezo wa kwanza toka Peter Snell wa New Zealand alipofanikiwa kutetea taji lake la michezo ya Olimpiki kwenye mita 800 mwaka 1964.

Katika mbio za wanawake mita 400, mwanariadha wa visiwa vya Bahamas Miller alishinda medali ya dhahabu kwa mtindo wa aina yake baada ya kuanguka sekunde chache tu kabla ya kuvuka mstari wa mwisho, akimshinda Mmarekani Allyson Felix kwa sekunde 49.44.

Shaunae Miller wa Bahamas kama anavyoonekana katika picha akijirusha wakati akimaliza mbio za mita 400 na kufanikiwa kushinda medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio, Brazil, 15AUG2016
Shaunae Miller wa Bahamas kama anavyoonekana katika picha akijirusha wakati akimaliza mbio za mita 400 na kufanikiwa kushinda medali ya dhahabu kwenye michezo ya Olimpiki ya Rio, Brazil, 15AUG2016 REUTERS/Fabrizio Bensch

Felix bingwa mara 4 wa michezo ya Olimpiki alijinyakulia medali ya fedha kwa kutumia muda wa sekunde 49.51 huku Mjamaika Shericka Jackson akimaliza kwenye nafasi ya tatu.

Katika tukio jingine la kustaajabisha kwenye michezi ya mwaka huu ya Rio, mchezaji Judo wa Misri Islam El Shehaby alijikuta akitimuliwa kwenye michezo ya mwaka huu baada ya kukataa kumpa mkono mpinzani wake Or Sason wa Israel.

Saa chache baada ya kumalizika kwa mchezo wake, kamati ya Olimpiki ilikashifu kitendo ilichosema sio cha kiuana michezo kilichooneshwa na mchezaji huyo wa Misri, ambapo ilitangaza kumfukuza.

Uamuzi wa kamati ya Olimpiki uliungwa mkono na kamati ya Olimpiki ya Misri ambayo nayo ilitangaza mara moja kumrudisha nyumbani mchezaji huyo katika raundi ya kwanza tu ya mchezo wake.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.