Pata taarifa kuu
RIADHA

Kenya kuendeleza ubingwa wa mbio za Mita 3000 kuruka viunzi na maji

Wanariadha wa Kenya wameendelea kutawala kwa kunyakua medali ya dhahabu katika mbio za Mita 3000  kuruka viunzi na maji, tangu mwaka 1968 kwa upande wa wanaume katika historia ya Michezo ya Olimpiki.

Wanariadha Ezekiel Kemboi (Kushoto) akiwa na wanaraidha wenzake baaada ya kushinda mbio za Mita 3000 kuruka maji na viunzi
Wanariadha Ezekiel Kemboi (Kushoto) akiwa na wanaraidha wenzake baaada ya kushinda mbio za Mita 3000 kuruka maji na viunzi IAAF
Matangazo ya kibiashara

Ushindi huu unaiweka Kenya kuendelea kushirika rekodi kuwa nchi bora katika mbio hizi katika michezo hii ya Olimpiki, mbio ambayo wanariadha huzunguka uwanja mara 7.

Hata hivyo, mwaka 1976 na 1980 Kenya haikushinda taji lolote baada ya kususia michezo ya Olimpiki kuunga mkono vita vya ubaguzi wa rangi nchini Afrika Kusini.

Tangu mwaka 1984, wakati Michezo hii ya Olimpiki ilipofanyika mjini Los Angeles nchini Marekani hadi mwaka 2012 wakati michezo hii ilipoandaliwa jijini London nchini Uingereza, Kenya imekuwa ikishinda medali ya dhahabu mfululizo.

Mwanariadha wa kwanza kunyakua medali hiyo alikuwa Amos Biwott,wakati wa michezo ya mwaka 1968 mjini Mexico City, nchini Mexico.

Wanariadha wengine ambao wameishindia Kenya medali ya dhahabu katika mbio hizi ni pamoja na Kipchoge Keino-1972 mjini Munich, Julius Korir-1984 mjini Los Angeles, Julius Kariuki -1988 mjini Seoul, Mathew Birir-1992 mjini Barcelona, Joseph Keter -1996 mjini Atlanta na Reuben Kosgei- 2000 mjini Sydney.

Bingwa anayeshikilia rekodi ya kushinda medali nyingi za dhahabu ni Ezekiel Kemboi mwaka-2004 mjini Athens na 2012 jijini London,sawa na Volmari Iso-Hollo kutoka Finland aliyeshinda mwaka 1932 na 1936.

Mwaka 2008, bingwa alikuwa ni Brimin Kipruto.

Wakati wa michezo ya mwaka 1992 na 2004, wanariadha wa Kenya walishinda medali zote tatu.

Ezekiel Kemboi amekwenda Brazil kwa lengo la kuweka historia, kuwa mwanariadha wa pekee kushinda medali tatu za dhahabu na kuendelea rekodi ya Kenya.

Mbali na Kemboi, wanariadha wengine katika mbio hii huko Brazil ni pamoja na Brimin Kipruto na Conseslus Kipruto.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.