Pata taarifa kuu
SOKA

CAF: Michuano ya lala salama kwa timu za vijana kufuzu fainali ya bara Afrika mwakani

Mechi za mzunguko wa mwisho kutafuta timu nane zitakazoshiriki katika fainali ya bara Afrika kwa wachezaji wasiozidi miaka 20 mwaka ujao nchini Zambia zinachezwa mwishoni mwa juma hili.

cafonline
Matangazo ya kibiashara

Michuano hii inachezwa nyumbani na ugenini na mshindi baada ya mechi hizo mbili atajikatia tiketi.

Zambia imefuzu kwa sababu wao ndio watakaokuwa wenyeji wa michuano hii.

Ukanda wa CECAFA unawakilishwa na Sudan peke baada ya mataifa mengine kushindwa kusonga mbele.

Leo Misri ambao ni mabingwa mara 4 ya michuano hii watakuwa wenyeji wa Angola ambao wamewahi kushinda taji hili mara 1 jijini Cairo.

Misri ilifuzu katika hatua hii baada ya kufanikiwa kuwashinda Rwanda kwa jumla ya mabao 3 kwa 2 kupitia mikwaju ya Penalti baada ya mechi za nyumbani na ugenini.

Angola nayo, ilitinga hatua hii baada ya kuishinda Gabon mabao 3 kwa 1.

Ratiba ya Jumamosi Julai 9 2016
Gambia vs Guinea
Burkina Faso vs Mali
Senegal vs Ghana

Ratiba ya Jumamosi Julai 10 2016
Sudan vs Nigeria
Lesotho vs Afrika Kusini
Cameroon vs Libya

Nigeria ndio mabingwa watetezi wa taji hili na wanashikilia rekodi ya kunyakua mataji 7 ya michuano hii mwaka 1983,1985,1987,1989,2005,2011 na 2015.

Misri wameshinda mara nne mwaka 1981,1991,2003,2013.

Ghana mara 3 mwaka 1993,1999,2009.

Cameroon (1995), Algeria (1979), Morocco(1997) na Angola (2001)

Mashindano yaliyopita yalifanyika nchini Senegal mwaka 2015.

 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.