Pata taarifa kuu
UGANDA-SOKA

Uganda: Timu ya taifa ya soka ya vijana yafuzu katika mzunguko wa 3

Timu ya taifa ya soka ya Uganda yenye wachezaji wasiozidi miaka 23 imefuzu katika mzunguko wa tatu kuwania tiketi ya kufuzu katika michuano ya Afrika itakayopigwa nchini Senegal kati ya tarehe 28 mwezi Novemba hadi tarehe 12 Desemba mwaka huu.

Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni.
Rais wa Uganda Yoweri Kaguta Museveni. RFI/Stéphanie Maupas
Matangazo ya kibiashara

Uganda ndio timu pekee inayowakilisha ukanda wa Afrika Mashariki na Kati katika michuano hiyo ya vijana na ilifuzu baada ya kuishinda Rwanda kwa jumla ya mabao 4 kwa 1.

Vijana hao wanaofahamika kwa jina maarufu Uganda Kobs, walipata ushindi nyumbani na ugenini. Mwishoni mwa juma lililopita wakiwa katika uwanja wa nyumbani wa Nakivubo jijiji Kampala vijana hao wlipata ushindi wa mabao 2 kwa 0.

Mabao ya Uganda yalitiwa kimyani na nahodha John Ssemazi na Faruku Miya kipindi cha pili cha mchuano huo.

Uganda sasa itamenyana na Misri nyumbani na ugenini mwezi katikati na mwisho wa mwezi ujao.

Kikosi cha timu ya Uganda :

Salim Magoola (G.K), Dues Bukenya, Brian Ochwo, Shafik Bakaki, Richard Kasagga, Derrick Tekkwo, Kizito Kezironi, Faruku Miya, Fahad Muhammed Tokko, John Ssemazi, Yunus Sentamu , Hassan Muhammed Fahad, Muzamiru Mutyaba,  Kezironi Kizito, Martin Kizza,  John Ssemazi, James Alitho (G.K), Tom Matisko, Abel Eturide na Ibrahim Kiyemba

Kikosi cha Rwanda :

Marcel Nzarora (G.K), Michel Rusheshangoga, Celestin Ndayishimye, Faustin Usengimana, Emery Bayisenge, Yannick Mukunzi, Bonfils Kabanda, Andrew Buteera, Djihad Bizimana, Xavio Nshuti, Isaie Songa, Michel Rusheshangoga, Fitina Ombarenga, Andrew Butera, Kevin Muhiire, Gahungu Habarurema (G.K), Bienvenue Mugenzi, Antoine Ndayishimiye , Abdoul Rwatubyaye na Robert Ndatimana.

Mataifa mengine ya Afrika Mashariki yaliyoondolewa katika michuano hii mbali na Rwanda ni Kenya na Somalia.

Mataifa manane yatakayoshiriki katika michuano ya Afrika na yatakayomaliza katika nafasi tatu bora yatafuzu katika michuano ya Olimpiki mwaka ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.