Pata taarifa kuu
SOKA-TP MAZEMBE-WYDAD

TP Mazembe yaondolewa katika michuano ya CAF

Klabu ya soka ya TP Mazembe imeondolewa katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kuelemewa na Wydad Casablanca ya Morocco.  Timu hizi mbili zimetoka sare ya bao 1 kwa 1 katika mchuano wa marudiano Jumatano jioni.

Mchezaji wa kimataifa na nahodha wa TP Mazembe, Joel Kimwaki, hana furaha kutokana na ushindi wa Wydad wa mabao 2-0 katika mechi ya awali..
Mchezaji wa kimataifa na nahodha wa TP Mazembe, Joel Kimwaki, hana furaha kutokana na ushindi wa Wydad wa mabao 2-0 katika mechi ya awali.. CARL DE SOUZA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Matokeo haya yanamaanisha kuwa Wydad Casablanca imefuzu katika hatua ya makundi kwa jumla ya mabao 3 kwa 1 baada ya ushindi wa mabao 2 kwa 0 katika mchuano wa kwanza wiki moja iliyopita.

Mashabiki wa TP Mazembe walikuwa na matumaini makubwa baada ya Salif Coulibaly kuwapa raha na matumaini kwa kuipa timu yake bao la ufunguzi katika dakika ya 28 kipindi cha kwanza.

Mazembe ambao walioneakana kucheza kwa kujituma mbele ya mashabiki wake, walishindwa kupita ngome ngumu ya wapinzani wao kipindi chote cha pili.

Mambo yalibadilika na yakawa mabaya zaidi katika dakika ya mwisho ya 90 baada ya Reda El Hajaoui kuisawazishia timu yake na hivyo kuyafanya matokeo hayo kuwa bao 1 kwa 1 hadi kipenga cha mwisho.

Mashabiki wa Mazembe waliofika kushuhudia mchuano huu wamerudi nyumbani wakiwa wamevunjika mioyo lakini hawajakata tamaa kwa sababu klabu yao sasa itacheza katika hatua ya mwondoano kutafuta taji la Shirikisho.

TP Mazembe wameondoka katika michuano hii baada ya kuweka rekodi ya kushinda mataji 5 mwaka 1967, 1968,2009,2010 na 2015.

Katika mechi nyingine ziliyopigwa Jumatano hii ni kati ya Al Ahly kutoka Misri ambao walikua wenyeji wa Yanga kutoka Tanzania. Hadi kipenga cha mwisho Yanga ilijikuta imeondolewa katika michuano ya klabu bingwa barani Afrika baada ya kufungwa mabao 2-1.

Kwa upande wao Enyimba wameibuka ushindi wa penati 4-3 dhidi ya Etoile du Sahel. Nao As Vita Club kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wamefaulu kuvuka daraja, licha ya kufungwa mabao 2-1 na Mamelod Sundowns.

Asec Mimosas wakabwagizwa na Al Ahli Tripoli kwa mabao 2-1. Hata hivyo Asec Mimosac Tripoli imefaulu kusonga mbele baada ya kukamilisha mabao 3-2.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.