Pata taarifa kuu
CAF-SOKA-AFRIKA

TP Mazembe yaangukia pua Casablanca

Mabingwa wa Ligi ya Mabingwa, TP Mazembe, wameshindwa kufanya vizuri ugenini na kujikuta wamelazwa kwa mabao 2-0 katika uwanja wa klabu ya Wydad mjini Casablanca, nchini Morocco, Jumamosi, Aprili 9.

Mchezaji wa kimataifa na nahodha wa TP Mazembe, Joel Kimwaki, usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili hii hana furaha kutoka na ushindi wa Wydad wa mabao 2-0.
Mchezaji wa kimataifa na nahodha wa TP Mazembe, Joel Kimwaki, usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili hii hana furaha kutoka na ushindi wa Wydad wa mabao 2-0. CARL DE SOUZA / AFP
Matangazo ya kibiashara

Matokeo ambayo ni mzigo mkubwa kwa klabu hii katika mechi ya marudiano. Wakati huo huo klabu ya Zesco United kutoka Zambia wamefanikiwa kupata ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Stade Malien, nchini Mali.

Onyo la mzunguko wa 16 halikua na funndisho lolote kwa klabu ya TP Mazembe. TP Mazembe hawakupata fundisho baada ya mechi yake iliyotangulia dhidi ya klabu maarufu ya Ethiopia ya St George, ambapo katika mchezo wa awali timu hizi mbili zilitoka sare ya kufungana mabao 2-2 na kisha mchezo wa marudiano TP Mazembe wakakubali kichapo cha 1-0. Kuna hatari TP Mazembe waage mashindano hayo waloishinda mara tano kabla ya hatua ya makundi. Klabu hii ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imeshindwa kufanya vizuri nchini Morocco dhidi ya Wydad, mabingwa wa Morocco, na kujikuta imepachikwa mabao 2-0 Jumamosi hii katika uwanja wa mjini Casablanca.

Katika dakika za mwanzo za mchezo huo, vijana wa Hubert Velud walikabiliwa na kibarua kigumu, kabla ya kupata ushindi huo.

Bao la kwanza la Wydad liliwekwa kimyani na beki Abdellatif Noussair dakika moja kutoka mapumziko. Kisha bao la pili lilifungwa katika ya 66 kupitia mkwaju wa penalti uliowekwa wavuni na Reda El Hajhouj baada ya Joel Kimwaki kufanya madhambi katika eneo la hatari.

Stade Malien yafungwa nyumbani

Katika mechi nyingine, katika hatua ya nane ya mtoano kwa mechi za awali klabu ya Zambia ya Zesco United ilipata ushindi mkubwa nchini Mali wa mabao 3-1 dhidi ya Stade Malien. Klabu ya Zambia ilikuja juu baada ya mchezaji wa Stade Malien, Diallo, kufanikisha kuifungia klabu yake bao la kwanza katika dakika ya 18. Bao la kwanza la Zesco United lilifungwa na mchezaji Mwelwa (katika dakika ya 44) na bao la pili na la tatu yalifungwa na Mbombo (katika dakika ya 75 na 85).

Klabu ya Algeria ya ES Setif ilifanikiwa kutoka sare na Al Merreikh kwa kufungana mabao 2-2, wakati ambapo Asec ya Abidjan ikipata fursa kubwa ya kuiadhibu Al Ahli mabao 2- 0.

►Jumamosi Aprili 9, 2016

Young Africans (Tanzania) - Al Ahly (Misri) 1-1

Al Merreikh (Sudan) - ES Setif (Algeria) 2-2

Zamalek (Misri) - Mouloudia Bejaia (Algeria) 2-0

Wydad Casablanca (Morocco) - TP Mazembe (DRC) 2-0

ASEC Mimosas (Côte d’Ivoire) - Al Ahly Tripoli (Libya) 2-0

Stade Malien (Mali) - Zesco Utd (Zambia) 1-3

►Jumapili Aprili 10, 2016

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.