Pata taarifa kuu

US Open: Richard Gasquet angia katika robo fainali

Bingwa wa pili nchini Ufaransa Richard Gasquet atacheza Jumatano wiki hii katika mashindano ya US Open mchuano wake wa pili wa robo fainali ya Grand Chelem ya mwaka huu, baada ya ushindi wake dhidi ya raia wa Jamhuri ya Czech, Tomas Berdych, kwa seti 2-6, 6-3, 6-4, 6-1, Jumatatu wiki hii.

Richard Gasquet wakati wa mechi alioshinda dhidi ya Tomas Berdych katika mzunguko wa 8 wa US Open Septemba 7, 2015 mjini New York.
Richard Gasquet wakati wa mechi alioshinda dhidi ya Tomas Berdych katika mzunguko wa 8 wa US Open Septemba 7, 2015 mjini New York. AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Gasquet ameungana na Jo-Wilfried Tsonga na Kristina Mladenovic, waliofanikiwa kuingia tangu Jumapili mwishoni mwa juma lililopita katika robo fainali ya mashindano ya US Open 2015.

katika raundi ijayo, Gasquet, aliyechukua nafasi ya 12 katika mashindano ya dunia, atamenyana na Mswisi Roger Federer, bingwa wa pili dunia na mshindi mara tano katika mashindano ya US Open, ambaye amemshinda Mmarekani John Isner, kwa seti 7-6 (7/0), 7-6 (8/6), 7-5.

Richard Gasquet, mwenye umri wa miaka 29, atacheza kwa mara ya nne robo fainali ya Grand Chalem tangu alipoanza mchezo huo, ikiwa ni mara ya pili katika mashindano ya US Open. Alishinda michezo yake mitatu iliyopita ya robo fainali, lakini aliuangushwa katika nusu fainali (Wimbledon mwaka 2007, US Open mwaka 2013, Wimbledon mwaka 2015).

Gasquet alianza vibaya mechi yake dhidi ya Berdych. Lakini baada ya kupoteza seti ya kwanza, alikuja juu na na kuondoa wasiwasi zote. Wachezaji wote hawa walikua sawa kwa michuano yao kwa ushindi mara sita kabla ya Gasquet kupata kumuangusha Berdych.

“ Nilianza vibaya mchezo huo, sikuhisi matumaini yoyote. Lakini baadae nilicheza vizuri, na mchezo ukawa rahisi. Nina furaha kumshinda Thomas, mmoja wa wachezaji bora wa kundi hili ", amesema Richard Gasquet.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.