TENNIS-MCHEZO
Tennis: Andy Murray na Vasek Pospisil wachuana leo
Michuano ya Tennis ya Wimbledon inaedelea leo na ni siku ya michuano ya robo fainali kwa upande wa wanaume.
Imechapishwa:
Matangazo ya kibiashara
Mchuano wa kwanza ni kati ya Andy Murray na Vasek Pospisil na baadaye bingwa mtetezi Novak Djokovich atamenyana na Marin Cilic.
Katika mchezo mwingine , Roger Federer anachuana na Gilles Simon, huku Stan Wawrinka akipambana na Richard Gasquet.
Kwa upande wa wanawake, Mmarekani Serena Williams alimshinda Victoria Azarenka kwa seti tatu za 3-6, 6-2, 6-3 na kufuzu katika hatua ya nusu fainali.
Serena naye anacheza leo Jumatano na Mrusi, Maria Sharapova katika mchuano wa nusu fainali.