Pata taarifa kuu
US OPEN-TENNIS-MCHEZO

US Open: Andy Murray aondolewa katika mzunguko wa 8

Bingwa watatu wa dunia Andy Murray ameangukia pua Jumatatu wiki hii katika michuano ya US Open baada ya kuburuzwa na raia kutoka Afrika Kusini, Kevin Anderson, ambaye amepata na fasi nzuri ya kucheza robo fainali yake ya kwanza kwa Grand Chelem mjini New York Jumatano wiki hii.

Andy Murray wakati wa mechi aliopoteza dhidi Kevin Anderson katika mzunguko wa8 wa mashindano ya US Open, Septemba 7, 2015 mjini New York
Andy Murray wakati wa mechi aliopoteza dhidi Kevin Anderson katika mzunguko wa8 wa mashindano ya US Open, Septemba 7, 2015 mjini New York AFP/AFP
Matangazo ya kibiashara

Murray ameshindwa kwa seti nne 7-6 (7/5), 6-3, 6-7 (2/7), 7-6 (7/0) baada ya saa nne na dakika kumi na tisa ya mchezo.

Andy Murray alikuwa na matumaini ya kufuzu kwa robo fainali ya michuano ya US Open, mashindano alioshinda mwaka 2012, kwa mwaka wa tano mfululizo, lakini Anderson amemshinda kutoka mwanzo hadi mwisho wa mchezo.

Anderson ambaye alichukua nafasi ya 14 katika msimu uliyopita amefanikiwa "mchezo mzuri zaidi katika kazi yake", kutokana na bidi aliyokua nayo.

Kutokana na umaarufu kwa ajili ya kufanya kwake vizuri, Anderson pia ameonekana akishambulia muda mrefu katika mchezo huo, kama inavyoonyesha idadi yake ya kuvutia ya pointi alizoshinda (81 kwa 49 dhidi ya Murray).

Pia alikuwa mkakamavu kwenye wavu kwa pointi 41 alizoshinda.

" Nina furaha kubwa kwa kuingia katika robo fainali na hasa kwa kumshibda mchezaji kama Andy. Nina furaha kuona nimevuka hatua kubwa katika kai yangu hii ", amesema Anderson, ambaye alishinda mwaka 2015 kwatuzo yake ya tatu ya ATP katika mji wa Winston Salem, muda mfupi kabla mashindano ya US Open.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.