Pata taarifa kuu
TANZANIA-SOKA

TFF : “ Mart Nooij hataachishwa kazi ”

Rais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF, Jamal Malinzi amesisitiza kuwa kocha wa timu ya taifa Mart Nooij hataachishwa kazi baada ya Misri kuishinda Taifa Stars mabao 3 kwa 0 katika mchuano wa kwanza kufuzu katika fainali za michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.

Dutchman Mart Nooij, kocha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ( Taifa Stars).
Dutchman Mart Nooij, kocha wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania ( Taifa Stars).
Matangazo ya kibiashara

Rais huyo wa TFF ametoa kauli hiyo jijini Dar es Salaam kutuliza shinikizo kutoka kwa wapenzi wa soka nchini humo wanamtaka kocha huyo kufutwa mara moja kutokana na matokeo mabaya.

Malinzi ameongeza kuwa wao kama viongozi wa soka hawawezi kukurupuka na uamuzi wa kumfuta kazi kocha Nooij na kwenda kinyume na makubaliano ya Kamati kuu ya soka nchini humo.

Mwezi uliopita, Kamati kuu ya TFF ilifikia uamuzi kuwa kocha Nooij atafutwa kazi iwapo Uganda itawaondoa katika michuano ya mzunguko wa kwanza ya kutafuta tiketi ya kufuzu katika michuano ya CHAN baina ya wachezaji wanaocheza soka nyumbani.

Tanzania inajiandaa kumenyana na Uganda katika mchuano wa kwanza wa kufuzu katika michuano hiyo ya CHAN itakayochezwa mwishoni mwa juma hili visiwani Zanzibar, kabla ya kurudiana baada ya majuma mawili jijini Kampala mapema mwezi ujao.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.