Pata taarifa kuu
MSUMBIJI-SOKA

Helder Muianga kocha mpya wa The Mambas

Beki wa zamani wa timu ya taifa ya soka ya Msumbiji Helder 'Mano Mano' Muianga amechukua mikoba ya Joao Chissano kuwa kocha wa timu ya taifa “The Mambas”.

Wakati Libya ikimenyana na Msumbiji katika michuano ya kufuzu ya Afcon 2012.
Wakati Libya ikimenyana na Msumbiji katika michuano ya kufuzu ya Afcon 2012. Reuters
Matangazo ya kibiashara

Kibarua cha Chissano kiliota nyasi baada ya kufungwa na Rwanda bao 1 kwa 0 katika mchuano wa kwanza wa kufuzu katika michuano ya mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.

Muianga alikuwa msaidizi wa Chissano katika mchuano huo wa mwishoni mwa juma lililopita jijini Maputo.

Kabla ya mchuano dhidi ya Rwanda, Chissano aliiongoza Msumbiji hadi katika fainali ya michuano ya Kusini mwa Afrika COSAFA mwisho uliopita na kufungwa na Namibia.g Chimodzi wa Malawi.

Kazi kubwa ya kocha mpya Muianga, ni kukiandaa kikosi cha wachezaji wanaocheza nyumbani katika michuano ya kufuzu katika mechi za CHAN dhidi ya Ushelisheli mwishoni mwa juma hili mjini Beira.

Muianga alipokuwa mchezaji licha ya kuichezea Msumbuji, aliwahi pia kucheza soka la kulipwa nchini Afrika Kusini na Hungary.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.