Pata taarifa kuu
CAF-SOKA-AFRIKA

Michuano ya Shirikisho barani Afrika mwishoni mwa juma hili

Michuano ya kwanza ya hatua ya makundi kuwania taji la Shirikisho barani Afrika CAF, zinachezwa mwishoni mwa juma hili katika viwanja mbalimbali barani Afrika.

Esperance Tunis - Tout Puissant Mazembe, katika fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa ya CAF mwaka 2010.
Esperance Tunis - Tout Puissant Mazembe, katika fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa ya CAF mwaka 2010. AFP PHOTO / FETHI BELAID
Matangazo ya kibiashara

Vilabu 16 vinashiriki katika hatua hii na vimepangwa katika makundi mawili na mshindi wa kwanza na wa pili atafuzu katika hatua ya nusu fainali.

Siku ya Jumamosi, Orlando Pirates ya Afrika Kusini itamenyana na Kaloum Star ya Guinea, huku Warri Wolves ya Nigerai ikiwa nyumbani kumenyana na AC Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Siku ya Jumapili, wawakilishi watatu wa Tunisia pia watakuwa viwanjani kutafuta ushindi.

Club Africain watamenyana na Al Ahly ya Misri, Etoile du Sahle dhidi ya Raja Casablanca ya Morroco na ES Tunis watakuwa ugenini kumenyana na Hearts of Oak ya Ghana.

Wawakilishi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo AS Vita Club watakuwa nyumbani jijini Kinshasa kumenyana na Stade Malien ya Mali, huku.

Sanga Balende kutoka mji wa Mbujimayi wataanza mchuano wao ugenini dhidi ya Zamalek ya Misri.

Wakati huo huo timu mbalimbali za taifa za mchezo wa soka katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati na kwingineko barani Afrika zinashuka dimbani mwishoni mwa juma hili kujipima nguvu katika michuano ya Kimataifa ya kirafiki.

Mataifa ya Afrika yanatumia michuano hii kujiandaa kwa mechi za kwanza kuwania nafasi ya kucheza katika fainali za kombe la mataifa bingwa barani Afrika mwaka 2017 nchini Gabon.

Siku ya Jumamosi, Kenya itamenyana na Tanzania jijini Kigai nchini Rwanda , huku Amavubi Stars nao wakiwa nyumbani watapambana na Sudan Kusini katika mchuano mwingine.

Niger watakabiliana na Gabon jijini Niamey, huku Guinea wakimaliza kazi na Chad.

Siku ya Jumapili, Ethiopia itaikaribisha Zambia huku Mali ikipepetana na Libya.

Mechi za kwanza zitapigwa kuanzia mwishoni mwa juma lijalo. Tanzania ambao wamejumuishwa katika kundi moja na Nigeria, Misri na Chad, wataanza kampeni zake dhidi ya mabingwa wa zamani Misri ugenini.

Kocha wa Taifa Stars Mholanzi Mart Nooij ameahidi kufanya vizuri katika michuano hiyo na kufuzu Gabon baada ya matokeo mabaya katika michuano iliyopita ya COSAFA baina ya mataifa ya Kusini mwa Afrika.

Kenya nayo inayofunzwa na kocha wa zamani wa Uganda Cranes Bobby Williamson, itaanza ugenini dhidi ya Congo Brazaville.

Mbali na Congo, Kenya imejumuishwa pia na Guinea Bissau na Zambia.

Uganda itaanza kazi na Bostwana katika kundi ambalo pia lina Burkina Faso na Comoros.

Rwanda nayo imepangwa na Ghana, Msumbiji na Mauritius na itaanza mchuano wake dhidi Msumbiji.

Leopard ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo ipo katika kundi moja na Angola, Jamhuri ya Afrika ya Kati na Madagascar.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.