Pata taarifa kuu
FIFA-CAF-BLATTER-SOKA

CAF yampongeza Blatter kwa kazi nzuri aliyoifanya

Shirikisho la soka barani Africa CAF, linasema Joseph Sepp Blatter atakumbukwa sana kwa kulisaidia bara la Afrika kuinua kiwango chake cha mchezo wa miguu.

Sepp Blatter ameliongoza Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kwa kipindi cha miaka 17.
Sepp Blatter ameliongoza Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) kwa kipindi cha miaka 17. REUTERS/Arnd Wiegmann
Matangazo ya kibiashara

Rais wa CAF ambaye pia ni naibu rais wa FIFA Issa Hayatou amesema kuwa CAF inaheshimu uamuzi wa Blatter kujiuzulu na inaunga mkono mabadiliko katika Shirikisho hilo.

Rais wa CAF, Issa Hayatou.
Rais wa CAF, Issa Hayatou. (Photo : Christophe Jousset / RFI)

“ Shirikisho la soka barani Afrika linaheshimu na kutambua kujiuzulu kwa Joseph Sepp Blatter ” , Hayatou ameema kupitia taarifa uliochapishwa katika mtandao wa CAF.

Tangu Sepp Blatter kutangaza kujiuzulu, viongozi wa vyama mbalimbali barani Afrika wamekuwa wakionesha masikitiko makubwa kwa hatua hiyo kwa kile wanachokisema kuwa Blatter ndiye aliyekuwa tegemeo lao.

Rais wa Shirikisho la soka nchini Kenya Sam Nyamweya amedokeza kuwa anaamini kuwa bara la Afrika litampigia kura mtu atakayependekezwa na Blatter.

“ Nimeshangazwa na hatua ya Blatter lakini tutaendelea kumuunga mkono na kumpigia kura yule atakayemchagua yeye ”, amesema Sam Nyamweya.

Nyamweya ameongezea kuwa, “ Tunaamini kuwa kura tulizompa Blatter, tutampa mgombea mwingine”.

Kiongozi huyo wa soka nchini Kenya amemsifu Blatter kwa kuisaidia Kenya kuanzia miradi ya kuinua soka hasa kwa vijana kwa kuhakikisha kuwa fedha zinapatikana.

Said El Mamry rais wa zamani wa Shirikisho la soka nchini Tanzania na mjumbe wa zamani wa FIFA na CAF amesema binafsi kama mtu aliyefanya kazi na Blatter kwa muda mrefu, hatua hiyo ni pigo kwa bara la Afrika.

“ Siku hizi ukitembea katika mataifa mbalimbali barani Afrika utaona Ofisi nzuri nzuri za mashirikisho ya soka, viwanja vya nyasi ya bandia na mambo mengine mazuri, hiyo ni kazi ya Blatter ”, amesema El Mamry.

Blatter alitangaza kujiuzulu siku ya Jumatatu kwa kile alichokisema kuwa hawezi kuendelea kuongoza kutokana na kundi la watu wanaompinga.

Uchaguzi mpya unatarajiwa kufanyika mwezi kati ya mwezi Desemba mwaka huu na mwezi Machi mwakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.