Pata taarifa kuu
FIFA-SOKA-RUSHWA-SHERIA

Chuck Blazer akiri kupokea rushwa

Vyombo vya sheria vya Marekani vimeweka wazi ushahidi wa Chuck Blazer, raia wa Marekani aliyekuwa katibu mkuu wa CONCACAF. Chuck Blazer ni mtu ambaye alisaidia kujenga shutuma za rushwa na kupinga dhidi ya uongozi wa FIFA.

Chuck Blazer alikuwa mjumbe wa kamati tendaji ya FIFA wakati alikuwa akifanya udukuzuzi kwa niaba ya FBI katika Shirikisho la Soka Dunia Fifa kwa kipindi cha miaka miwili.
Chuck Blazer alikuwa mjumbe wa kamati tendaji ya FIFA wakati alikuwa akifanya udukuzuzi kwa niaba ya FBI katika Shirikisho la Soka Dunia Fifa kwa kipindi cha miaka miwili. AFP PHOTO / PETER KOHALMI
Matangazo ya kibiashara

Chuck Blazer, ambaye amekiri kuwa ana hatia ya kupokea rushwa, huenda makosa yake yakafutwa. Chuck Blazer alisaidia kwa kiasi kikubwa Idara ya ujasusi ya Marekani FBI kwa kufichua utaratibu wa rushwa uliyokua ukitumiwa kwenye Shirikisho la Soka Duniani.

Kwa mujibu wa mwandishi wa RFI, jijini Washington, Anne-Marie Capomaccio, Chuck Blazer amekiri kupokea rushwa. Katika maelezo yake, mwenyekiti wa zamani wa Shirikisho la Soka Amerika ya Kaskazini CONCACAF amebaini kwamba hakupokea rushwa hiyo mwenyewe bali wanahusika pia maafisa kadhaa wa Shirikisho la Soka Duniani (FIFA).

" Natambua kuwa mimi na maafisa wengine wa FIFA, tulipokea rushwa katika uteuzi wa Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa michuano ya Kombe la Dunia mwaka 2010 ", Chuck Blazer ameilezea FBI.

Chuck Blazer amekubali pia, akiwa pamoja na maafisa wengine wa FIFA, kuwa walipokea rushwa mwaka 1998. Amekubali pia kuwa kuna ujanja fulani waliyotumia kwa kuruhusu kurushwa moja kwa moja hewani michuano ya Kombe la Dunia na michuano yote ya Amerika ya Kaskazini tangu mwaka 1996. Chuck Blazer ameeleza kwa undani kuhusu namna walivyokua wakitumiwa fedha hizo kupitia benki mbalimbali au kwa kutumia hundi walizokua wakipewa kwa mkono.

Chuck Blazer alikuwa akifanya udukuzi kwa niaba ya FBI katika Shirikisho la Soka Dunia FIFA kwa kipindi cha miaka miwili. Alikubali kuwafanyia kazi viongozi wa Marekani baada ya kugunduliwa na mamlaka ya kodi kwa kushindwa kulipa kodi kwa mamilioni ya fedha aliyopitisha mlango wa nyuma kwa kipindi cha miaka ishirini na moja akiwa kama Katibu mkuu mtendaji wa Concacaf, ambalo ni Shirikisho la Soka la Amerika ya Kaskazini, Amerika ya Kati na Caribbean.

Kati ya mwaka 2011 na 2013, wakati alikua bado mjumbe wa kamati tendaji ya FIFA, Chuck Blazer alikua akibebelea chombo kidogo cha kurekodi sauti ambaco alikua akikificha kwenye funguo zake gari. Chuck Blazer alirekodi mazungumzo zaidi ya mia moja, ambayo yote yaliwekwa kwenye faili iliyofunguliwa na Mwendesha mashtaka wa wilaya ya Mashariki ya New York, Loretta Lynch, ambaye ni waziri wa sheria wa Marekani tangu Aprili 27.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.