Bayern na Barcelona zajitupa uwanjani
Michuano ya nusu fainali za Kombe la Mabingwa barani Ulaya katika mechi ya marudiano inatazamiwa kuchezwa Jumanne jioni wiki hii, kati ya Barcelona ya Uhispania na Bayern Munich ya Ujerumani.
Imechapishwa:
Bayern Munich leo Jumanne jioni inajaribu kubadilisha matokeo ya mabao 3-0 kipigo ilichopata wiki iliyopita dhidi ya Barcelona katika mchezo wa kwanza wa nusu fainali ya za Kombe la Mabingwa barani Ulaya.
Bayern ambayo itawakosa wachezaji wake muhimu katika mchezo huo kutokana na kukumbwa na matatizo makubwa ya majeruhi katika kikosi chake itakuwa katika uwanja wake wa Allianz Arena ikiikaribisha Barcelona usiku wa leo.
Katika mechi ya awali, mabao mawili ya Barcelona yaliwekwa wavuni na Lionel Messi. Bao la kwanza liliingizwa katika dakika ya 76, huku bao la pili liwekwa wavuni katika dakika ya 80.
Bao la tatu lilifungwa na Neymar katika dakika 1 za nyongeza baada ya dakika 90 za mchezo.
Katika mechi ya awali Barcelona ilionekana kutawala mpira katika kipindi cha pili hasa pale Messi alipoifungulia klabu yake bao la kwanza.
Katika kipindi cha kwanza klabu zote mbili zilikua sare, na zilionekana zikicheza vizuri na zikiwa na nguvu sawa.
Hadi kipenga cha mwisho Bayern Munich imejikuta ikiangukia pua.