Pata taarifa kuu
SOKA-UEFA-BARCELONA-BAYERN MUNICH

Bayern Munich yapata kichapo cha mabao 3-0

Michuano ya nusu fainali za Kombe la Mabingwa barani Ulaya imeendelea kwa siku ya pili Jumatano wiki hii, kati ya Barcelona ya Uhispania na Bayern Munich ya Ujerumani.

Lionel Messi aliyeifungia klabu yake ya Barcelona mabao mawili dhidi ya Bayern Munich, Mei 6 mwaka 2015. de la Liga (30 buts), le 8 mars 2015.
Lionel Messi aliyeifungia klabu yake ya Barcelona mabao mawili dhidi ya Bayern Munich, Mei 6 mwaka 2015. de la Liga (30 buts), le 8 mars 2015. Reuters / Gustau Nacarino
Matangazo ya kibiashara

Hadi dakika 90 za mchezo huo Barcelona imekua ikiongoza kwa mabao matau dhidi ya Bayern Munich.

Mabao mawili ya Barcelona yamewekwa wavuni na Lionel Messi. Bao la kwanza limeingizwa katika dakika ya 76, huku bao la pili liwekwa wavuni katika dakika ya 80.

Neymar mchezaji wa Barcelona kutoka Brazili aliyefunga bao la tatu dhidi ya Bayer Munch.
Neymar mchezaji wa Barcelona kutoka Brazili aliyefunga bao la tatu dhidi ya Bayer Munch. Reuters / Albert Gea

Bao la tatu limefungwa na Neymar katika dakika 3 za nyongeza baada ya dakika 90 za mchezo. Barcelona imeonekana kutawala mpira katika kipindi cha pili hasa pale Messi alipoifungulia klabu yake bao la kwanza.

Katika kipindi cha kwanza klabu zote mbili zilikua sare, na zimeonekana zikicheza vizuri na zikiwa nguvu sawa. Klabu hizo zimeonyesha mchezo mzuri licha ya kutobahatika kufungana katika kipindi cha kwanza,

Hadi kipenga cha mwisho Bayern Munich imejikuta ikiangukia pua.

Katika mchuano wa kwanza wa nusu fainali za Kombe la Mabingwa barani Ulaya kati ya Juventus ya Italia na Real Madrid ya Uhispania uliochezwa Jumanne usiku wiki hii, Juventus waliibuka mshindi wa mabao 2-1 dhidi ya Real Madrid.

Juventus walikua wenyeji wa mchuano huo. Mchezo wa marudiano utachezwa Mei 13 katika uwanja wa Bernabeu, mjini Madrid.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.