Pata taarifa kuu
UEFA-MICHEZO-SOKA

Bayern Munich na Barcelona zatinga nusu fainali

PSG haikufanikiwa kufanya vizuri katika uwanja wa Barcelona katika mchuano wa marudiano baada ya kufungwa katika mchuano wa awali uliyochezwa katika uwanja wa Parc des Princes, nchini Ufaransa kwa mabao 3-1.

Neymar mchezaji wa Barcelona kutoka Brazili aliyefunga mabao mawili dhidi ya PSG ya Ufaransa.
Neymar mchezaji wa Barcelona kutoka Brazili aliyefunga mabao mawili dhidi ya PSG ya Ufaransa. Reuters / Albert Gea
Matangazo ya kibiashara

Katika mchuano wa marudio kati ya Barcelona na PSG uliyochezwa Jumanne Aprili 21, hadi dakika tisini za mchezo PSG imejikuta imebwagizwa mabao 2-0, na kupelekea Barcelona kutinga katika nusu fainali.

Licha ya kurudi uwanjani kwa Ibrahimovic na Verratti, ambao waliondolewa katika mchuano wa awali uliyochezwa Ufaransa, katika uwanja wa Parc des Princes, PSG imeshindwa mchezo, na kupoteza matumaini ya kuibuka mshindi.

Bao la kwanza la Barcelona limewekwa wavuni katika dakika ya 14, huku bao la pili likiingizwa wavuni katika dakika ya 34. Mabao yote hayo mawili ya Barcelona yamewekwa kimyani na mchezaji wa Brazil Neymar.

Kwa upande wake Bayern Munich baada ya kuchezea kichapo cha mabao 3-1 katika mechi ya awali dhidi ya Porto FC ugenini, hatimaye wachezaji wa klabu hii walikuja juu na kugeza matokeo ya awali dhidi ya Porto. Hadi dakika tisini za mchezo Porto FC imejikuta imeangukia pua kwa kufungwa mabao 6-1.

Kwa sasa klabu za Bayern Munich ya Ujerumani na Barcelona ya Hispania zimetinga nusu fainali katika ligi ya Mabingwa barani Ulaya, huku PSG ya Ufaransa na Porto FC zikiaga mashindano hayo.

Leo Jumatano ni zamu ya Real Madrid mabingwa watetezi dhidi ya Athletico Madrid zote kutoka nchini Uhispania, na Monaco ya Ufaransa dhidi ya Juventus ya Italia.

Baada ya michuano ya robo fainali, droo ya michuano ya nusu fainali itafanyika tarehe 24 mwezi huu kabla ya kuanza kwa michuano ya nyumbani na ugenini tarehe 5 na 6 mwezi ujao huku michuano ya marudiano ikiwa ni tarehe 12 na 13 mwezi ujao.

Fainali itachezwa tarehe 6 mwezi Juni katika uwanja wa Olympiastadium jijini Berlin nchini Ujerumani .

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.