Pata taarifa kuu
SOKA-MICHUANO YA KLABU BINGWA UEFA

Real Madrid yaimenya Liverpool bao moja kwa nunge

Mabingwa watetezi wa taji la klabu bingwa barani Ulaya UEFA, Real Madrid ya Uhispania imefuzu katika hatua ya kumi na sita bora baada ya kuishinda Liverpool ya Uingereza bao 1 kwa 0.

Kikosi cha wachezaji wa Real Madrid, baada ya kuimenya Liverpool kwa bao moja kwa nunge.
Kikosi cha wachezaji wa Real Madrid, baada ya kuimenya Liverpool kwa bao moja kwa nunge. (Photo : Reuters)
Matangazo ya kibiashara

Beki ya Liverpool ilikuwa imara lakini bao la mapema la Karim Benzema katika dakika ya 27 ya mchuano huo lilitosha kuipa ushindi Real Madrid.

Kwa ushindi huo wa jana Jumanne Novemba 4, Real Madrid inaongoza kundi la B kwa alama 12, ikifuatwa na Basel ikiwa na alama 6, huku Liverpool ikiwa na alama 3.

Klabu nyingine ambayo pia imefuzu katika hatua ya kumi na sita bora ni Borussia Dortmund ya Ujerumani baada ya kuishinda Galatasaray ya Uturuki kwa mabao 4 kwa 1 na wanaongoza kundi lao la D kwa alama 12.

Katika matokeo mengine, Arsenal wakiwa nyumbani walitoka sare ya mabao 3 kwa 3 na Anderlecht ya Ubelgiji, huku Benfica ikiishinda Monaco bao 1 kwa 0.

Jumatano Novemba 5 michuano hiyo hiyo itaendelea, ambapo Manchester City ya Uingereza itakua katika uwanja wao wa nyumbani wa Etihad kucheza na CSKA Moscow ya Urusi, Bayern Munich ya Ujerumani itakuwa katika uwanja wao wa Allianz Arena kupambana na Roma ya Italia.

Barcelona watakuwa ugenini kumenyana na Ajax, huku Maribor wakichuana na Chelsea ya Uingereza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.