Pata taarifa kuu
LIGI KUU YA WINGEREZA

Liverpool yaanza vizuri

Kwa kipindi cha miaka 5 kutokua uwanja katika michuano ya ligi kuu ya Uingereza, klabu ya Liverpool jumanne wiki hii imeshangaza wengi baada ya kuifunga Ludogorets mabao (2-1).

Liverpool yatamba uwanjani baada ya kuifunga Ludogorets mabao 2-1.
Liverpool yatamba uwanjani baada ya kuifunga Ludogorets mabao 2-1. REUTERS/Nigel Roddis
Matangazo ya kibiashara

Liverpool imepata ushindi huo baada ya kiungo wa klabu hiyo Mario Balotelli, ambaye ni raia wa Itali kutikisa wavu wa lango la Ludogorets katika dakika ya 81 ya mchezo, kabla ya nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard kuingiza bao la pili baada ya Ludogorets kusawazisha kwa mkwaju wa penalti katika dakika ya 90 na kupelekea klabu Ludogorets kukata tamaa.

Hata hivo bao hilo la kwanza liloingizwa wavuni na Balotelli, limeelezewa kua la kifahari, baada ya mchezaji huyo nyota kuwapa funzo wachezaji wawili wa Ludogorets na kujikuta mpira ukicheza wavuni.

Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, baada ya kuingiza bao la pili dhidi ya Ludogorets.
Nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, baada ya kuingiza bao la pili dhidi ya Ludogorets. Liverpool FC

Nahodha wa Liverpool Steven Gerrard amebaini kwamba timu yake inakabiliwa na kazi ya ziada ili kupata nafasi nzuri hususan kupata ushindi dhidi ya timu za bara Ulaya ili iweze kushamiri barani Ulaya kama ilivyokuwa mwaka 2005.

Hata hivo nahodha wa Liverpool, Steven Gerrard, amesema kwamba bado wana kazi kubwa ya kuishinda FC Basel, ambayo jumanne wiki hii imeshindwa kufanya vizuri baada ya kuchapwa na Real Madrid mabao 5-1.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.