Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Alejandro Sabellah atangaza kikosi kamili cha wachezaji 23 wa timu ya taifa ya Argentina

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Argentina, Alejandro Sabella ametangaza kikosi chake cha wachezaji 23 watakaoambatana na timu hiyo kuelekea nchini Brazil tayari kushiriki fainali za kombe la dunia 2014 huku akimuacha mchezaji tegemeo Ever Banega kwenye kikosi chake.

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Argentina, Alejandro Sabellah
Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Argentina, Alejandro Sabellah afa.com
Matangazo ya kibiashara

Miongoni mwa wachezaji wengine waliotemwa kwenye kikosi hiki ni pamoja na kiungo, Jose Sosa anayekipiga na klabu ya Atletico Madrid na Nicolas Otamendi anayecheza kwenye klabu ya Atletico Mineiro.

Wengine walioachwa ni pamoja na mshambuliaji wa Werder Bremen Franco Di Santo, Lisandro Lopez, Gabriel Mercado na Fabian Rinaudo.

Wachezaji mahiri ambao wametemwa kwenye kikosi cha kocha Sabella ni pamoja mchezaji aliyenunuliwa kwa dau kubwa na klabu ya Tottenham ya Uingereza Erik Lamela pomoja na mshambuliaji wa klabu ya Juventus, Carlos Tevez na Javier Pastore anayekipiga na klabu ya Paris St-Germain.

Mchezaji Carlos Tevez ambaye ameachwa na kocha wake wa timu ya taifa, Sabellah
Mchezaji Carlos Tevez ambaye ameachwa na kocha wake wa timu ya taifa, Sabellah REUTERS/Phil Noble

Katika hatua ya kushangaza kocha Sabella amemjumuisha kwenye kikosi chake mchezaji majeruhi Fernando Gago, Augusto Fernandez na Andel Di Maria ambao wote anategemea watakuwa vizuri kabla ya kuanza kwa michuano ya mwaka huu juma lijalo.

Timu hiyo ya Argentina ambayo iko kwenye kundi F pamoja na timu ya taifa ya Iran, Bosnia na Nigeria, itaundwa na walinda mlango, Sergio Romero (Sampdoria), Mariano Andujar (Catania), Agustin Orion (Boca Juniors).

Walinzi ni pamoja na, Pablo Zabaleta (Manchester City), Federico Fernandez (Napoli), Ezequiel Garay (Benfica), Marcos Rojo (Sporting Lisbon), Hugo Campagnaro (Inter Milan), Martin Demichelis (Manchester City), Jose Basanta (Monterrey).

Kiungo ni pamoja na, Javier Mascherano (Barcelona), Fernando Gago (Boca Juniors), Lucas Biglia (Lazio), Ricardo Alvarez (Inter Milan), Augusto Fernandez (Celta Vigo), Angel Di Maria (Real Madrid), Maxi Rodriguez (Newell's Old Boys), Enzo Perez (Benfica).

Huku safu ya ushambuliaji ikitarajiwa kuongozwa na, Lionel Messi (Barcelona), Gonzalo Higuain (Napoli), Sergio Aguero (Manchester City), Rodrigo Palacio (Inter Milan), Ezequiel Lavezzi (Paris St-Germain).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.