Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Carlos Tevez kumshtaki Kocha wa Manchester City Roberto Mancini

Mshambuliaji wa Kimataifa wa Argentina anayekipiga katika Klabu ya Manchester United Carlos Tevez anatarajiwa kumshtaki Meneja wa Timu hiyo Roberto Mancini kwa kosa la kumkashfu kwa mujibu wa uchunguzi ambao umefanyika kutokana na kosa alilotenda kwenye mchezo dhidi ya Bayern Munich.

REUTERS/Phil Noble
Matangazo ya kibiashara

Tevez amechukua uamuzi huo baada ya Klabu ya Manchester City kumlima faini ya kuchukua mishahara yake ya majuma manne baada ya ucnguzi kubaini kuwa alikataa kucheza kwenye mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya dhidi ya Bayern Munich.

Mchezaji huyo ambaye amekuwa katika wakati mgumu ameshauriwa kumshtaki Tevez kutokana na maneno yake ya kashfa ambayo ameyatoa kwenye mkutano na waandishi wa habari uliofanyika baada ya mchezo huo.

Tevez amepewa siku kumi na nne kuweza kukata rufaa kupinga uamuzi huo wa yeye kukatwa mshahara wake kwa kosa la kugomea kucheza licha ya kocha wake Mancini kumtaka aingie kwenye mchezo huo kuisaidia Manchester City iliyokuwa nyuma kwa magoli mawili.

Mshambuliaji huyo iwapo atashindwa kwenye rufaa yake ndani ya Klabu ya Manchester City atakuwa na nafasi ya kuelekeza malalamiko yake kwenye Mahakama ya Ligi Kuu Nchini Uingereza.

Uongozi wa Manchester City ambao bado unamkataba wa miaka mitatu na Tevez umesema ataendelea kuwepo na wala hatouzwa kama amnavyo mwenyewe amekuwa akishinikiza Timu hiyo kufanya.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.