Pata taarifa kuu
KOMBE LA DUNIA BRAZIL 2014

Kikosi cha timu ya taifa ya Ecuador chatangazwa, yumo mchezaji wa Man utd, Antonio Valencia

Kiungo wa pembeni wa klabu ya Manchester United ya nchini Uingereza, Antonio Valencia amejumuishwa kwenye kikosi cha wachezaji 23 wanaounda kikosi kamili cha timu ya taifa ya Ecuador itakayoshirikia fainali za kombe la dunia nchini Brazil mwaka huu.

Kiungo mshambuliaji wa timu ya taufa ya Ecuador, Antonio Valencia
Kiungo mshambuliaji wa timu ya taufa ya Ecuador, Antonio Valencia REUTERS
Matangazo ya kibiashara

Vlancia mwenye umri wa miaka 28 ameichezea timu yake ya Man utd mara 44 na licha ya mchango wake kwenye timu alishuhudia wakimaliza kwenye nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu ya Uingereza.

Kiungo wa timu ya Stuttgart ya Ujerumani, Carlos Gruezo mwenye umri wa miaka 19 pia amejumuishwa kwenye kikosi cha mwisho cha kocha Reinaldo Rueda.

Kiungongo mwingine ni Segundo Castillo ambaye licha ya majeraha ya goti aliyokuwa nayo bado amejumuishwa kwenye kikosi hiki cha wachezaji 23 wanaoelekea nchini Brazili.

Kocha Rueda pia amewaacha wachezaji watatu waliokuwa wanacheza ligi kuu ya nyumbani kwenye kikosi chake cha wachezaji 23 licha ya kuwa aliwajumuiya kwenye kikosi cha wachezaji 30 wa awali, wachezaji hao ni washambuliaji, Cristian Penilla, Angel Mena and Armando Wila.

Wachezaji wengine walioachwa ni pamoja na Jhon Narvaez, Fortuna Dusseldorf, Cristian Ramirez, Pedro Quinonez na Oswaldo Minda.

Timu hii iko kwenye kundi E pamoja na Uswis, Ufaransa na Honduras.

Wachezaji kamili wanaounda kikosi cha timu ya taifa ya Ecuador ni pamoja na walinda mlango, Maximo Banguera (Barcelona SC), Alexander Dominguez (LDU Quito), Adrian Bone (El Nacional).

Walinzi ni, Frickson Erazo (Flamengo), Jorge Guagua, Oscar Bagui, Gabriel Achilier (all Emelec), Walter Ayovi (Pachuca), Juan Carlos Paredes (Barcelona SC).

Viungo ni pamoja na, Segundo Castillo (Al-Hilal), Carlos Gruezo (Stuttgart), Renato Ibarra (Vitesse Arnhem), Cristian Noboa (Dynamo Moscow), Luis Saritama (Barcelona SC), Antonio Valencia (Manchester United), Edison Mendez (Independiente Santa Fe), Fidel Martinez (Tijuana), Michael Arroyo (Atlante).

Huku upande wa washambuliaji wataongozwa na, Felipe Caicedo (Al-Jazira), Jefferson Montero (Morelia), Joao Rojas (Cruz Azul), Jaime Ayovi (Tijuana), Enner Valencia (Pachuca).

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.