Pata taarifa kuu
UINGEREZA

Ferguson aeleza siri ya ushindi, awasifu Valencia na Young

Kocha wa Manchester United ya Uingereza Sir Alex Fugerson ameelezea furaha yake baada ya kupata ushindi katika mchezo wa mabao 2-0 dhidi ya Blackburn, hiyo jana.

RFI
Matangazo ya kibiashara

Kwa ushindi huo Manchester United wameendelea kujiweka imara katika nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini Uingereza baada ya Antonio Valencia na Ashley Young kufunga magoli katika 81 na 86 kwa mfuatano.

Matokeo ya jana yanaifanya United kulinda matarajio yao ya kupata taji la tano katika kipindi cha misimu sita.

Ferguson amesema kuibuka na ushindi katika dakika za mwisho ni muhimu kwa kuwa ni mafanikio na mfano mzuri kwenye historia ya klabu yao.

Akimsifu Valencia, Fergurson amesema ikiwa asingejaribu kupiga mikwaju asingebaini kuwa unaweza kufunga namna ile na alitumia nguvu zake nyingi kufanikisha upatikanaji wa goli.

Juma lijalo Man U itajitupa uwanjani na QPR wakati Wigan itakakwaana na Aston villa

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.