Pata taarifa kuu

Vita vya Gaza: Israeli yapanga tarehe ya mashambulizi Rafah, mazungumzo yanaendelea

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu alisema siku ya Jumatatu kwamba tarehe imepangwa kwa ajili ya mashambulizi katika mji wa Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza. Wakati wengi serikalini hawaungi mkono kutumwa kwa wanajeshi wa Israel huko Gaza, Marekani inapinga "uvamizi wowote wa kijeshi" huko Rafah. Marais wa Ufaransa na Misri pamoja na mfalme wa Jordan  wamesema katika makala ya Gazeti la Le Monde kuunga mkono juhudi zozote "kwa ajili ya kusitisha mapigano mara moja huko Gaza".

Picha hii iliyotolewa na Ikulu ya rais wa Misri inamuonyesha Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi (katikati), akiwa na Mkuu wa Idara ya Ujasusi Meja Jenerali Abbas Kamel (wa pili kulia), wakikutana na Mkurugenzi wa CIA William Burns (wa pili kushoto) na Balozi wa Marekani mjini Cairo, Herro Mustafa Garg (kushoto). Ikulu ya Rais mjini Cairo, Aprili 7, 2024.
Picha hii iliyotolewa na Ikulu ya rais wa Misri inamuonyesha Rais wa Misri Abdel Fattah al-Sisi (katikati), akiwa na Mkuu wa Idara ya Ujasusi Meja Jenerali Abbas Kamel (wa pili kulia), wakikutana na Mkurugenzi wa CIA William Burns (wa pili kushoto) na Balozi wa Marekani mjini Cairo, Herro Mustafa Garg (kushoto). Ikulu ya Rais mjini Cairo, Aprili 7, 2024. © AFP PHOTO / HO / EGYPTIAN PRESIDENCY
Matangazo ya kibiashara

Ushindi dhidi ya kundi la Hamas “unahitaji kuingia Rafah na kukomeshwa kwa vita vya kigaidi. Mashambulizi yatafanyika, tarehe imeshapangwa," Waziri Mkuu wa Israeli alitangaza katika taarifa ya video bila kutoa maelezo zaidi. Waziri mkuu anakabiliwa na mvutano na mzozo ndani ya serikali yake, anabainisha mwandishi wetu mjini Jerusalem, Michel Paul.

Kwa upande mmoja, Waziri wa Ulinzi Yoav Gallant anabaini kwamba Israel iko "katika wakati mwafaka wa " kutakakuachiliwa kwa mateka. Kwake yeye, anaona miezi ya vita na matokeo kwenye uwanja wa vita upande wa Israel unawezesha Israeli kuharakisha katika mchakato wa kufanya maamuzi. Maoni ya waziri huyu, ambayo mara nyingi humetengwa ndani ya serikali, yanaibua hisia kutoka mrengo wa kulia ambao pia unatilia shaka kutumwa tena kwa jeshi huko Gaza.

Uamuzi huu unakosolewa haswa na mawaziri Bezalel Smotrich na Itamar Ben-Gvir, ambaye anasisitiza kwenye mitandao ya kijamii kwamba kama Benyamin Netanyahu ataamua kumaliza vita dhidi ya Hamas bila ya mashambulizi makubwa huko Rafah, "atakuwa amemaliza mamlaka ya kuhudumu kama Waziri Mkuu". Baraza la mawaziri la usalama linatarajiwa kukutana Jumanne jioni kuchukua, inasemekana, "maamuzi mazito". Mkutano ambao unaahidi kuwa na shughuli nyingi.

Upinzani wa Marekani

Kwa upande wake, Marekani ilithibitisha kwa nguvu Jumatatu upinzani wake kwa operesheni yoyote kubwa ya Israel huko Rafah, kusini mwa Ukanda wa Gaza. "Tumeweka wazi kwa Israeli kwamba tunaamini kwamba uvamizi mkubwa wa kijeshi wa Rafah utakuwa na athari mbaya kwa raia hawa na hatimaye utadhuru usalama wa Israeli," msemaji wa wizara ya amambo ya Ne ya Marekani, Matthew Miller, aliwaambia waandishi wa habari.

"Sio tu kuhusu Israeli kutuonyesha mpango. "Tuliweka wazi kwao kwamba tunaamini kuna njia bora zaidi ya kufikia lengo halali, ambalo ni kupunguza, kusambaratisha na kushinda vita vya Hamas ambavyo vimesalia Rafah," Miller aliongeza.

Kusitishwa kwa mapigano mara moja huko Gaza

Washington na nchi nyingi zinahofia usalama wa Wagaza zaidi ya milioni 1.5 ambao wamepata hifadhi katika eneo hili lililo kusini kabisa mwa Ukanda wa Gaza, karibu na mpaka uliofungwa na Misri. Katika kesi hii, upinzani huu unashirikiwa na Marais Emmanuel Macron na Abdel Fattah al-Sissi na Mfalme wa Jordan, Abdallah II katika safu iliyochapishwa katika gazeti la Le Monde.

"Vita vya Gaza na mateso makubwa ya kibinadamu lazima vikome mara moja," wanasema viongozi hao watatu. Wanatoa wito wa "usuluhisho wa serikali mbili", "chaguo pekee la kuaminika la kudhamini amani na usalama kwa wote na kuhakikisha kwamba sio Waisraeli au Wapalestina wanaopaswa kufufua hali ya kutisha ambayo imewakumba tangu mashambulizi ya Oktoba 7, 2023."

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.