Pata taarifa kuu

Miezi sita ya vita huko Gaza na malengo ambayo hayajafikiwa kwa Israeli

Imepita miezi sita Jumapili hii, Aprili 7, tangu mashambulizi ya Hamas yalipotokea ambayo yalisababisha vifo vya watu zaidi ya 1,100 nchini Israel na kusababisha vita vya Israel katika Ukanda wa Gaza, idadi ya waliouawa imezidi 33,000 kwa mujibu wa mamlaka ya eneo hilo . Kimkakati, Israel haijafikia malengo yake ya vita.

Operesheni ya ardhini ambayo Israel inatishia kuzindua huko Rafah kusini mwa eneo hilo bado haijaanza na, miezi sita baada ya mashambulizi, mazungumzo ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka na wafungwa hayajazaa matunda.
Operesheni ya ardhini ambayo Israel inatishia kuzindua huko Rafah kusini mwa eneo hilo bado haijaanza na, miezi sita baada ya mashambulizi, mazungumzo ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka na wafungwa hayajazaa matunda. REUTERS - Lisi Niesner
Matangazo ya kibiashara

Kuondoa Hamas kutoka Ukanda wa Gaza na kuhakikisha kuachiliwa kwa mateka wa Israeli. Haya ndiyo malengo ya vita yanayodaiwa na Israel. Lakini, baada ya miezi sita ya mzozo, viongozi wakuu wa Hamas huko Gaza, kuanzia na Yahya Sinouar, bado hawajapatikana. Marwan Issa ndiye mtendaji pekee wa ngazi za juu wa kundi al Hamas aliyeuawa katika eneo la Palestina.

Swali la mateka huamsha hasira na jinamizi kati ya familia zao

Operesheni ya ardhini ambayo Israel inatishia kuzindua huko Rafah kusini mwa eneo hilo bado haijaanza na, miezi sita baada ya mashambulizi, mazungumzo ya kusitisha mapigano na kuachiliwa kwa mateka na wafungwa hayajazaa matunda. Ni watatu tu walioachiliwa na jeshi la Israel; 130 bado wako katika Ukanda wa Gaza, ambao chini ya mia moja wanaaminika kuwa hai. Na kupitia tu mazungumzo kwa njia isiyo ya moja kwa moja na Hamas ambapo Israeli iliweza kufanikiwa kupata mateka zaidi ya mia moja waliyokuwa wanashikiliwa na Hamas mwezi Novemba mwaka uliyopita.

Katika Kongamano la Familia za Watekaji huko Tel Aviv, lililoundwa siku moja baada ya Oktoba 7 ili kusaidia familia za mateka na kuweza kufikisha mbali sauti zao, wengi wamenyamanzishwa. Ni wale tu waliothubutu kujitoa mhanga ambao wanaendelea na kudai ndugu zao kurejeshwa nyumbani, kama vile Gil Dickmann. Binamu yake Carmel Gat anashikiliwa mateka huko Gaza. “Tunawataka warudi nyumbani sasa. Hili ndilo jambo muhimu zaidi. Tusipowapigania watafia huko. Ni lazima tuwapiganie. Na nina hakika kwamba kutokana na uhamasishaji wetu, tutapata njia ya kuwakomboa,” alisema.

Lakini nchini Israeli, serikali imefanya kuangamiza Hamas lengo lake kuu la vita. Kuachiliwa kwa mateka kunakuja katika hatua ya pili. "Haikubaliki," anapinga kijana huyo mwenye umri wa miaka 31. “Waketi kwenye meza ya mazungumzo na wafanye kinachohitajika kukomesha haya yote. Kuna njia ya kuwakomboa mateka. Tayari tumetoa baadhi yao mwishoni mwa mwezi wa Novemba mwaka jana, kutokana na makubaliano ambayo yalihitimishwa. Kabla ya hapo, hakuna mtu aliyeamini kuwa inawezekana. Kwa hivyo, viongozi wetu lazima waache kupoteza wakati. Lazima watie saini makubaliano mapya ya kuwarudisha mateka, na hatimaye tunaweza kujenga upya maisha yetu. Kwa sababu hapa tuna ndoto mbaya. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.