Pata taarifa kuu

Mauaji ya wafanyakazi wa WCK Gaza: Jeshi la Israel lakiri kufanya mfululizo wa 'makosa makubwa'

Jeshi la Israel lilidai Ijumaa hii, Aprili 5, kwamba lilikuwa likimlenga "mshambuliaji wa Hamas" aliyekuwa akifyatua risasi kutoka kwenye paa la moja ya lori za misaada wakati lilipowaua wafanyakazi saba wa shirika lisilo la kiserikali la Kimarekani la World Central Kitchen huko Gaza, na kukiri kuwa limefanya mfululizo wa "makosa makubwa". Mara tu baada ya taarifa hizi, WCK ilitaka kuundwa kwa tume huru ya uchunguzi.

Gari ambalo wafanyakazi wa World Central Kitchen (WCK) wakiwemo wageni, waliuawa katika shambulio la anga la Israel huko Deir Al-Balah, katikati mwa Ukanda wa Gaza, Aprili 2, 2024.
Gari ambalo wafanyakazi wa World Central Kitchen (WCK) wakiwemo wageni, waliuawa katika shambulio la anga la Israel huko Deir Al-Balah, katikati mwa Ukanda wa Gaza, Aprili 2, 2024. © Ahmed Zakot / Reuters
Matangazo ya kibiashara

Wafanyakazi hawa wa kibinadamu waliuawa Jumatatu jioni, Aprili 1, katika Ukanda wa Gaza na mashambulizi matatu ya Israeli yaliyotekelezwa katika muda wa dakika nne kwenye msafara wao.

Timu inayoendesha ndege zisizo na rubani iliyohusika na mashambulizi hayo ilifanya "kosa la kiutendaji katika kutathmini hali" baada ya kuona "mshambuliaji wa Hamas" akipiga risasi kutoka kwenye paa la moja ya lori za misaada ambazo wasaidizi wa shirika lisilo la kiserikali la Marekani la World Central Kitchen (WCK) waliokuwa wakisindikiza, kwa mujibu wa uchunguzi wa ndani wa jeshi. Jeshi, ambalo linarejelea "ukiukaji wa taratibu za kawaida za uendeshaji", pia limetambua kuwa WCK ilionyesha na kutangaza ramani ya barabara itakazotumia kwa msafara wake, lakini askari waliosimamia mashmbulizi hawakuwa nayo mkononi.

Katika mkutano na waandishi wa habari katika makao makuu ya jeshi huko Tel Aviv, maafisa wakuu wa Israeli wameonyesha waandishi wa habari kanda ya video ya ndege isiyo na rubani inayoonyesha "afisa wa Hamas" akiungana na msafara wa WCK ukisafiri kuelekea Gaza usiku wa Jumatatu kuamkia siku ya Jumanne muda mfupi baada ya nne usiku (saa za ndani).

Wimbi la hasira

Nembo kubwa za WCK zilipamba paa za magari hayo, lakini kamera ya ndege isiyo na rubani haikuweza kuziona gizani, amesema Jenerali mstaafu Yoav Har-Even, anayeongoza uchunguzi huo. "Hilo lilikuwa jambo kuu katika msururu wa matukio," almesema.

Vifo vya wasaidizi hao wa kibinadamu vilizusha wimbi la hasira, huku Rais wa Marekani Joe Biden akimwomba Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu siku ya Alhamisi kuagiza "kusitishwa mara moja kwa mapigano" wakati wa mazungumzo ya simu. Aprili 5 Naibu Waziri wa Mambo ya Nje wa Poland, kwa upande wake, alibaini kwamba aliomba Israeli kufanya "uchunguzi wa jinai" kwa "mauaji".

"Tunataka kuundwa kwa tume huru yenye jukumu la kuchunguza mauaji ya wenzetu," imesema WCK katika taarifa muda mfupi baada ya taarifa ya jeshi la Israel ambayo ilibaini kwamba "haiwezi kuchunguza kwa uaminifu makosa iliyofanya Gaza," imeongeza shirika hilo lisilo la kiserikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.