Pata taarifa kuu

Vita huko Gaza: 'Jeshi la Israeli likiingia Rafah, itakuwa janga'

Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametoa idhni kwa mazungumzo mapya kuhusu usitishwaji vita huko Gaza. Lakini wakati huo huo, eneo la Palestina lililozingirwa limekuwa likishambuliwa bila kuchoka na jeshi la Israel kwa karibu miezi sita. Huko Gaza, habari za mazungumzo haya kwa ajili ya kusitisha mapigano zinapokelewa kwa tahadhari kubwa.

Vijana wa Kipalestina wakiwa katika jengo lililoporomoka baada ya shambulio la angala Israel katika kambi ya Maghazi, Machi 29, 2024.
Vijana wa Kipalestina wakiwa katika jengo lililoporomoka baada ya shambulio la angala Israel katika kambi ya Maghazi, Machi 29, 2024. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Siku zinakwenda, vita vinaendelea na matumaini ya kusitishwa kwa mapigano yanazidi kupungua katika Ukanda wa Gaza, anasema mwandishi wetu mjini Jerusalem, Sami Boukhelifa. Usitishwaji wa mapigano ulitarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwezi wa Ramadhani. Tarehe 29 Machi hii ni Ijumaa ya tatu ya mwezi mtukufu kwa Waislamu na hakuna kilichobadilika.

Mabomu ya Israel bado yanaendelea kudondoshwakwenye ardhi ya Palestina. "Kutoka kaskazini hadi kusini, hakuna eneo ambalo halijalengwa na mashambulizi ya jeshi la Israeli," Asma anaiambia RFI. Huyu raia wa Gaza kwa sasa ni mkimbizi huko Rafah. "Ulikuwa usiku mgumu. Kulikuwa na milipuko ya mabomu karibu nasi. Walishambulia na kuharibu nyumba huko Rafah. Uvamizi wa Israel katika muda wa saa 24 zilizopita umesababisha vifo vya watu 71, kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas. Kwa jumla, zaidi ya Wapalestina 32,623 waliuawa katika shambulio la kulipiza kisasi la Israeli, kulingana na chanzo hicho.

Tangu mwezi Oktoba na kufuatia shambulio la Hamas lililosababisha vifo vya zaidi ya 1,000 nchini Israel, jeshi la anga la Israel limekuwa likishambulia kwa mabomu eneo lote la Palestina. Lakini askari wa ardhini wanafanya mashambulizi ya hatua. Kaskazini mwa Gaza, Jiji la Gaza, Khan Younes... Lengo la mwisho ni Rafah, ambapo wapiganaji wa Hamas watakuwa wamejikita, kulingana na Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu. "Tunatumai kwamba hakutakuwa na shambulio la ardhini huko Rafah. Ili tuweze kukaa hapa hadi mwisho wa vita. Jeshi likiingia Rafah, litakuwa janga,” anaeleza Asma. Takriban Wagaza milioni 1.5 wamepata hifadhi, kwa amri ya jeshi la Israel, huko Rafah.

Mazungumzo mapya

Wakati huo huo, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ametoa idhni siku ya Ijumaa kwa mazungumzo mapya ya usitishwaji vita katika eneo la Wapalestina la Gaza. Katika miezi ya hivi karibuni, vikao kadhaa vya mazungumzo vimefanyika kupitia wapatanishi wa kimataifa - Misri, Qatar na Marekani - lakini bila kuzaa matunda, wahusika wakuu wakituhumiana kila mmoja kwa kuzuia mazungumzo.

Tangu kuanza kwa vita, ni suluhu la wiki moja pekee ambalo lilianzishwa mwishoni mwa mwezi wa Novemba. Iliweesha kuachiliwa kwa karibu mateka mia moja waliotekwa nyara wakati wa shambulio la Oktoba 7 badala ya wafungwa wa Kipalestina waliokuwa wamefungwa na Israel.

Siku ya Ijumaa, Israel pia ilisema haikuhusika katika usambazaji wa chakula huko Gaza, ikiyashutumu mashirika ya Umoja wa Mataifa kwa kushindwa kusimamia kiasi cha misaada inayofika huko kila siku. Pia imehoji ripoti ya Umoja wa Mataifa ambayo ulionya juu ya hatari ya njaa katika eneo la Palestina, ikiushtumu kuwa una "makosa". Huku zikikabiliwa na hila za misaada inayowasili kwa nchi kavu kupitia Rafah, inayodhibitiwa vikali na Israel, nchi kadhaa zinadondosha chakula kila siku, Lakini hii bado haitoshi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.