Pata taarifa kuu

Hamas kutathmini pendekezo la kusitisha mapigano kwa wiki sita

Hamas ambayo inapambana katika vita na Israel katika Ukanda wa Gaza inatathmii pendekezo la hatua tatu la kusitisha mapigano, ambalo la kwanza linatoa usitishaji vita kwa muda wa wiki sita, chanzo ndani ya kundi hilo la Hamas kimeliambia shirika la habari la AFP siku ya Jumatatu.

Raia wa Gaza waliokuwa wamepata hifadhi huko Rafah wanarejea Khan Younes baada ya matangazo kutoka kwa jeshi la Israel, Jumapili Aprili 7, 2024.
Raia wa Gaza waliokuwa wamepata hifadhi huko Rafah wanarejea Khan Younes baada ya matangazo kutoka kwa jeshi la Israel, Jumapili Aprili 7, 2024. AFP - MOHAMMED ABED
Matangazo ya kibiashara

Awamu hii ya kwanza pia inatoa nafasi ya kuachiliwa kwa mateka wa Israel kwa kubadilishana na Wapalestina 800 hadi 900 wanaoshikiliwa katika jela za Israel, kuingia kwa lori 400 hadi 500 za msaada wa chakula kwa siku na kurejea nyumbani kwa wakazi wa kaskazini mwa Ukanda wa Gaza walioyoyahama makaazi yao kutokana na vita, kilmesema chanzo hiki.

Kiongozi wa upinzani wa Israel atoa wito wa makubaliano ya kuwaachilia mateka

"Mkataba wa kutekwa nyara unaweza kufikiwa. Ni mpango mgumu, ni mpango ambao huenda hatupendi, lakini unawezekana na kwa hivyo ni lazima ufanyike," Yair Lapid amewaambia waandishi wa habari baada ya mazungumzo na mkuu wa diplomasia ya Marekani Antony Blinken. "Watu hawa lazima warudi kwa familia zao," ameongeza.

Mashambulizi katika mji wa Rafah 

Ushindi dhidi ya vuguvugu la Kiislamu la Palestina "unahitaji kuingia Rafah na kukomeshwa kwa vita vya kigaidi huko. Hili litafanyika - kuna tarehe," waziri mkuu wa Israel alisema katika taarifa yake ya video.

Israel imesema kwa wiki kadhaa kwamba imedhamiria kufanya mashambulizi ya ardhini huko Rafah licha ya onyo kutoka kwa nchi za magharibi ambayo inahofia usalama wa zaidi ya watu milioni 1.5 wa Gaza ambao wamepata hifadhi katika eneo hili kusini mwa Ukanda wa Gaza karibu na mpaka uliofungwa na Misri.

Maafisa kadhaa wa Israel wamethibitisha mpango huu wa mashambulio tangu tangazo la Jumapili la kuondolewa kwa wanajeshi wa Israel kutoka Khan Younes, mji mwingine ulioko kusini mwa eneo la pwani unaohusika na mapigano kwa miezi kadhaa.

Matarajio ya kusitishwa kwa mapigano yanaweka shinikizo kwa Benjamin Netanyahu, ambaye washirika wake wa muungano wanaonya dhidi ya kufanya maafikiano mengi katika vita dhidi ya Hamas. "Iwapo Waziri Mkuu ataamua kumaliza vita bila kushambulia Rafah ili kushinda Hamas, hatakuwa na mamlaka ya kuendelea kuwa waziri mkuu," Waziri wa Usalama wa Taifa Itamar Ben Gvir ameonya Jumatatu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.