Pata taarifa kuu

Waangalizi wa Umoja wa Mataifa wajeruhiwa Lebanon: Israel yailaumu Hezbollah

Jeshi la Israel limesema siku ya Jumatano kwamba mlipuko uliojeruhi waangalizi watatu wa Umoja wa Mataifa na mkalimani wao wa Lebanon siku ya Jumamosi kusini mwa Lebanon, mpakani na Israel, ulihusishwa na kilipuzi kilichowekwa awali katika eneo hilo na Hezbollah. 

Maafisa wa Idara ya huduma za dharura wako kazini baada ya shambulio la anga la Israeli katika kijiji cha Hebbarye, kusini mwa Lebanon, Jumatano Machi 27, 2024.
Maafisa wa Idara ya huduma za dharura wako kazini baada ya shambulio la anga la Israeli katika kijiji cha Hebbarye, kusini mwa Lebanon, Jumatano Machi 27, 2024. © AP/Mohammed Zaatari
Matangazo ya kibiashara

"Kwa mujibu wa taarifa zilizopo kwa jeshi, mlipuko wa Machi 30 (...) ulitokea baada ya gari la UNIFIL (Kikosi cha Muda cha Umoja wa Mataifa) kilipuzi kilichowekwa hapo awali na Hezbollah kutoka Lebanon, jeshi la Israel linabaini kwenye ukurasa wake wa X, na ambalo baada ya tukio hilo lilithibitisha kutofanya shambulio katika mkoa huo.

Hvi karibuni wasaidizi wa shirika lisilo la kiserikali la Marekani ambalo hupeleka chakula katika Ukanda wa Gaza unaotishiwa na njaa waliuawa katika shambulio la Israel siku ya Jumatatu Aprili 1, mwanzilishi wake alitangaza, huku Hamas ikiripoti wahanga watano, ikiwa ni pamoja na wageni wanne.

Marekani, ambayo inazidi kujitenga na mshirika wake Israel baada ya karibu miezi sita ya vita katika Ukanda wa Gaza, ilitangaza siku ya Jumatatu kuwa "imefadhaishwa sana" na tukio hili. "Tumehuzunishwa na tunasikitishwa sana shambulio hili," msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa Adrienne Watson amesema kwenye mtandao wa kijamii wa X. "Wafanyakazi wa misaada lazima walindwe wanapotoa misaada inayohitajika, na tunaitaka Israel kuchunguza mara moja kilichotokea," ameongeza.

Jeshi la Israel limesema "linachunguza tukio hilo la kusikitisha kwa kiwango cha juu zaidi ili kuelewa mazingira" na linahakikisha kwamba "lilifanya kazi kwa karibu na WCK" kwa usambazaji wake wa misaada. Shirika la World Central Kitchen linahusika katika kutuma msaada kwa boti kutoka Cyprus hadi Gaza na kujenga gati ya muda katika eneo la Palestina lililozingirwa. Boti ya kwanza ilishusha shehena yake hapo katikati ya mwezi Machi chini ya usimamizi wa jeshi la Israel.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.