Pata taarifa kuu
MAZUNGUMZO-AMANI

Gaza: Mazungumzo yaanza tena kati ya Israel na Hamas mjini Cairo, suala la kusitisha mapigano

Mazungumzo kati ya Israel na Hamas yameanza tena mjini Cairo, nchiniMisri ili kufikia mwafaka huko Gaza na makubaliano ya kuwaachilia mateka. Kaei kubwa iko upande wa Hamas, inasema Marekani. Kundi hili la wanamgambo la Hamas kutoka Palestina linasema makubaliano ya kusitisha mapigano yanaweza kutiwa saini ndani ya "saa 24, 48" ikiwa Israel itakubali matakwa yake.

Wapalestina wanatembea katikati ya magofu ya kambi ya Jabaliya, Februari 29, 2024.
Wapalestina wanatembea katikati ya magofu ya kambi ya Jabaliya, Februari 29, 2024. AP - Mahmoud Essa
Matangazo ya kibiashara

Ni mwendelezo wa mvutano kuhusu upatanishi wa makubaliano mapya kati ya Israel na Hamas, anasema mwandishi wetu mjini Jerusalem, Michel Paul. Suala hilo linasalia kuwa suluhu na kubadilishana mateka na wafungwa wa Kipalestina kwa ajili ya mwezi mtukufu wa Ramadhan ambao utaanza baada ya wiki moja. Israel, asubuhi ya leo Machi 3, inasalia imara katika misimamo yake ambayo inaweza kurejelewa baadaye kidogo leo wakati wa mkutano wa kila wiki wa Baraza la Mawaziri huko Jerusalem.

Maafisa wa Israel wanasubiri majibu ya Hamas kwa mfumo elekezi ulioanzishwa katika mkutano wa Paris. Katika hatua hii, Israel inasitisha ushiriki wake katika mazungumzo yanayoendelea Cairo na kuitaka Hamas kwanza itoe orodha ya mateka inayowashikilia huko Gaza na ambao bado wako hai.

Makubaliano ya wiki sita?

Hakuna jibu kwa ripoti za matumaini kutoka Washington kwamba Israeli "imekubali pendekezo la kusitisha mapigano, kwa maneno yaliyotumiwa na afisa mkuu wa Marekani. Kwenye meza ya mazungumzo kuna suluhu ya wiki sita na pia kuachiliwa kwa mateka wanaochukuliwa kuwa walio hatarini zaidi, wagonjwa, waliojeruhiwa, wazee na wanawake. Kwa mtazamo wa Waisraeli kwa hiyo bado inasubiri.

Kwa upande wa Wapalestina, "ikiwa Israel itakubali matakwa ya Hamas, ambayo ni pamoja na kuwarejesha Wapalestina waliokimbia makazi yao kaskazini mwa Gaza na kuongezeka kwa misaada ya kibinadamu, hii inaweza kufungua njia ya makubaliano (ya mapatano) ndani ya saa 24 au 48 zijazo. ” amesema afisa mkuu mnamo Machi 3 asubuhi, ambaye hakutaka jina lake litajwe, wakati mazungumzo yalipangwa kufanyika Jumapili huko Cairo, rshirika la habari la AFP limeripoti.

Wakati huo huo, mashambulizi kadhaa ya anga yalilenga miji ya Khan Younes na Rafah kusini wakati wa usiku, kulingana na mwandishi wa shirika la habari la AFP huko Gaza. Serikali ya Hamas pia imesema moto mkubwa wa mizinga ulilenga Jabaliya, Beit Hanoun, Zeitoun na Tal al-Hawa kaskazini. Katika takriban miezi mitano, operesheni za kijeshi za Israel zilizoanzishwa kulipiza kisasi shambulio ambalo halijawahi kushuhudiwa la Hamas nchini Israel mnamo Oktoba 7 zimesababisha vifo vya watu 30,410 katika Ukanda wa Gaza, ambao ni raia walio wengi, Wizara ya Afya imesema leo Jumapili. Imeripoti vifo 90 ndani ya saa 24, wakiwemo watu 14 wa familia moja katika shambulio la anga huko Rafah.

Njaa "isiyoepukika"

Mgogoro huo pia umesababisha maafa ya kibinadamu na njaa "isiopukika" kwa watu milioni 2.2, idadi kubwa ya wakazi wa Gaza, kulingana na Jens Laerke, msemaji wa OCHA, shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.