Pata taarifa kuu

Marekani: Tunatumaini ya kufikiwa makubaliano ya kusitishwa mapigano Gaza wiki ijayo

Marekani imesema ina matumaini ya kufikiwa makubaliano ya kusitishwa mapigano kati ya Israel na Hamas hivi karibuni. Rais wa Marekani Joe Biden ametaja uwezekano wa mapatano kufikia wiki ijayo, wakati ambapo mzozo wa kibinadamu unatishia kuwa baa la njaa huko Gaza.

Mashambulizi ya Israel yamesababisha vifo vya watu 29,782 huko Gaza, wengi wao wakiwa raia, kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas.
Mashambulizi ya Israel yamesababisha vifo vya watu 29,782 huko Gaza, wengi wao wakiwa raia, kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas. © AFP
Matangazo ya kibiashara

Misri, Qatar, Marekani, Ufaransa na mataifa mengine yamekuwa yakijaribu kujadili makubaliano mapya ya usitishaji wa mapigano kati ya Israel na Hamas kwa wiki kadhaa. Kwa mujibu wa chanzo cha habari ndani ya kundi la wanamgambo wa Kipalestina wa Hamas, majadiliano hayo yanahusu usitishaji wa mapigano wa wiki sita unaohusishwa na kuachiliwa kwa mateka wanaoshikiliwa na Hamas na wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa na Israel, pamoja na kuingia kwa kiasi kikubwa cha misaada ya kibinadamu huko Gaza.

"Nina matumaini kwamba kufikia Jumatatu ijayo tutakuwa na usitishaji mapigano," rais wa Marekani alisema Jumatatu usiku mjini New York. "Mshauri wangu wa usalama wa taifa ananiambia kuwa tuko karibu, hata kama bado halijafanyika," ameongeza. Afisa mmoja wa Israel ambaye hakutaka kutajwa jina, aiambia tovuti ya habari ya Ynet kwamba "wanaelekea pazuri".

Tamim ben Hamad Al-Thani, Amir wa Qatar, nchi ambayo ni kitovu cha juhudi za mazungumzo na ambayo ni inawaopa hifadhi viongozi wa Hamas, anaanza ziara ya kiserikali ya siku mbili mjini Paris siku ya Jumanne, ofisi ya rais wa Ufaransa imetangaza. Lakini Benjamin Netanyahu alisisitiza tena Jumapili kwamba Israel itaanzisha hivi karibuni operesheni ya ardhini dhidi ya Rafah, kuwezesha, "ushindi kamili" dhidi ya Hamas katika "wiki chache". Makubaliano ya usitishaji mapigano "yachelewesha" tu uoperesheni hii, alisisitiza.

Siku ya Jumatatu jeshi la Israel liliwasilisha kwa baraza la mawaziri la vita la Israel "mpango wa kuwahamisha watu kutoka maeneo ya mapigano katika Ukanda wa Gaza, pamoja na mpango wa operesheni za siku zijazo", kulingana na ofisi ya waziri mkuu, bila kutoa maelezo yoyote kuhusu wapi raia watakimbilia.

Siku ya Jumatatu Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres alionya kwamba mashambulizi dhidi ya mji wenye wakazi wengi wa Rafah, ambapo Israel inataka kuwahamisha raia ili kushinda Hamas mara moja, "itakuwa kizingiti kikubwa" kwa programu za misaada.

Rafahambayo iko kwenye mpaka uliofungwa na Misri, kusini mwa Gaza, ni kituo pekee cha kuingilia misaada ya kibinadamu kwa Ukanda wa Gaza, unaowapa hifadhi Wapalestina milioni 1.4 na ambako mapigano yamepamba moto tangu karibu miezi mitano kati ya jeshi la Israel na Hamas.

Mashambulizi ya Israel yalisababisha vifo vya watu 29,782 huko Gaza, wengi wao wakiwa raia, kulingana na Wizara ya Afya ya Hamas. Vita vilianza Oktoba 7 wakati makomando wa Hamas walipoanzisha mashambulizi ambayo hayajawahi kushuhudiwa kusini mwa Israel, na kusababisha vifo vya takriban watu 1,160, wengi wao wakiwa raia, kulingana na hesabu ya shirika la habari la AFP kutoka kwa data rasmi ya Israeli.

Wakati wa shambulio hilo, takriban watu 250 walitekwa nyara na kupelekwa Gaza. Kulingana na Israel, mateka 130 bado wanazuiliwa katika jimbo hilo, 31 kati yao wanaaminika wamefariki.

Waziri mkuu wa Israel anakabiliwa na shinikizo zinazoongezeka za umma kuhusu hatma ya mateka ambao bado wanashikiliwa huko Gaza na maandamano dhidi ya serikali yake yameanza tena. Waisraeli wanatarajiwa kupiga kura siku ya Jumanne katika uchaguzi wa manispaa, ambao ulipangwa kufanyika mwishoni mwa mwezi Oktoba lakini uliahirishwa mara mbili kutokana na vita.

Wagaza wakabiliwa na njaa

Serikali za kigeni na wasaidizi wa kibinadamu wameongeza maonyo dhidi ya mashambulizi dhidi ya Rafah ambayo yatasababisha hasara nyingi na kuzidisha maafa ya kibinadamu. Wapalestina huko Gaza wameliambia shirika la habari la AFP kuhusu kulazimishwa kula majani, malisho ya mifugo, na hata kuchinja wanyama kwa ajili ya chakula huku misafara adimu ya misaada inayofika kaskazini ikiporwa na wakazi.

"Tunakufa kwa njaa," Abdallah Al-Aqra, 40, mkimbizi katika Jiji la Gaza, ameliiambia shirika la habari la AFP. Amesema jeshi liliwapiga risasi "watu wenye njaa waliokuwa wakijaribu kupata unga" ulioletwa na lori la misaada siku ya Jumapili.

Mashirika mawili yasiyo ya kiserikali, Amnesty International na Human Rights Watch (HRW), yaliishutumu Israel siku ya Jumatatu kwa kuendelea kuzuia kuingia kwa msaada wa kibinadamu Gaza licha ya ombi kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Haki (ICJ) mwezi Januari. Siku ya Jumatatu jeshi la Jordan lilisema lilidondosha siku kadhaa mfululizo misaada ya kibinadamu, chakula na vifaa vingine "moja kwa moja kwa wakazi wa Palestina" katika Ukanda wa Gaza uliozingirwa, ikiwa ni pamoja na ndege ya jeshi la Ufaransa.

Serikali ya Mamlaka ya Ndani ya Palestina iliwasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa Rais Mahmoud Abbas siku ya Jumatatu, huku miito ikiongezeka ya mageuzi ya uongozi wa kisiasa wa Palestina katika Gaza "baada ya vita". Tangu mwaka 2007, uongozi wa Palestina umegawanyika kati ya Mamlaka ya Palestina ya Mahmoud Abbas, ambayo ina uwezo mdogo katika Ukingo wa Magharibi, eneo linalokaliwa kwa mabavu tangu 1967 na Israel, huku Hamas ikidhibiti Ukanda wa Gaza.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.